Contact Us

Use the form on the right to contact us.

Or use the information below to contact our main office in Dar es Salaam or Arusha.

Main office:

P.o. box 12772 Dar Es Salaam, Tanzania

Phone: +255 786 197 412

E-mail: salesmanager.somabiblia@gmail.com

Publishing department

Postal address: P.o. Box 2696 Arusha, Tanzania

Phone: + 255 787392951

E-mail: publishing.somabiblia@gmail.com

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

KALENDA YA UKUTANI 2017 MASHINDANO YA PICHA

Habari kutoka Soma Biblia

KALENDA YA UKUTANI 2017 MASHINDANO YA PICHA

Anne Gihlemoen

Je kuna nukuu ya mstari wa Biblia iliyo muhimu kwako? Je unapenda kupiga picha? Labda ungependa kuchanganya vyote viwili na kutuma vichapishwe kwenye Soma Biblia Kalenda ya Ukutani Mwaka 2017.

Hakika hili ni shindano la kusisimua kwa wasomaji wetu wote wa Biblia.

  • Tafuta nukuu uipendayo ya Biblia uiambatanishe na picha yako nzuri.
  • Kisha tuma picha na nukuu kwetu kabla ya Juni tarehe 3, hapo utakuwa mmoja wa washiriki katika mashindano haya.
    Picha nne nzuri za mwanzo na nukuu zake zitapata nafasi ya kuchapishwa kwenye KALENDA YA UKUTANI 2017.

Kila mmoja mwenye kamera anaweza kushiriki!

Tuma picha yako na nukuu kabla Juni tarehe 3 kwenda:
editor.somabiblia@gmail.com

Masharti na vigezo vya mashindano:

1.      Kila mtu isipokuwa wafanyakazi wa Soma Biblia anaruhusiwa kushiriki haya mashindano.

2.      Picha lazima iwe inafundisha na ioane na nukuu kutoka Biblia. Nukuu isiwe zaidi ya maneno 40. Washiriki wanapaswa kujua kuwa waamuzi wanahaki ya kubadili nukuu kama wataipenda picha na kukuta inaoana zaidi na nukuu nyingine ya Biblia.

3.      Picha na nukuu ya Biblia lazima itumwe kwa barua pepe au kupitia huduma ya messenger katika ukurasa wetu wa facebook.

4.      Kila anayetuma picha au nukuu lazima aambatanishe majina kamili, namba ya simu na anuani, wakati wa kutuma.

5.      Kila mtu (mtu mzima au mtoto vile vile) atakaye tokea kwenye picha lazima awe amekubali kupigwa picha, na awe amekubali kuwa unaipeleka picha kwenye mashindando. Lazima pia wajulishwe kuwa kama picha itachaguliwa, itachapishwa katika Soma Biblia kalenda ya ukutani 2017, na pia inaweza kutumika kwa matumizi mengine na idara ya uchapishaji ndani ya Soma Biblia.

6.      Soma Biblia inayo haki ya kuchapisha picha na nukuu zitakazochaguliwa iwe kama zilivyo au zikiwa zimehaririwa, katika Soma Biblia kalenda ya ukutani 2017 na machapisho mengine. Picha zitakazochapishwa zitapata sifa kwa kuambatanishwa na jina la aliyepiga picha.

7.      Watakaotuma ndio wahusika wapicha walizopiga. Ni jukumu la washiriki kuhakikisha wana umiliki halali wa picha wanazotuma.

8.      Atakaye vunja sheria, kuchafua, au kuletakero katika ushiriki ataondolewa.

9.      Watakaotuma lazima wawajulishe waamuzi kama picha zimehaririwa au kufanyiwa ujanja waaina yoyote.

10.  Washindi watachaguliwa na waamuzi ikijumuisha Publishing manager, Editor na Layout wanaohusika ndani ya Soma Biblia. Na washindi watapewa taarifa.

11.  Washindi nne watapokea zawadi ya vitabu vyenye thamani ya 30 000 TSH, Kalenda ya Ukutani Mwaka 2017 tano na Soma Biblia Kalenda 2017 tano.