TWENDE 2/2023 - Linapatikana
Cathbert Msemo
YESU APENDA WATOTO
MPENDWA MSOMAJI
Ukisoma katika Biblia utakuta mistari mingi inayotaja neno UPENDO. Ni kwa sababu Mungu ndiye asili ya upendo na Biblia ni neno la Mungu.
Yohana 3:16 inasema, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele". Mungu anatupenda sana. Kwa njia ya Yesu Kristo ali-tukomboa sisi kutoka katika utumwa wa dhambi, na anatuhesabia haki bure. Huu ni upendo mkubwa sana sivyo?
Swali ni, Je, wewe unampenda Mungu? Unawapenda na wenzako pia? Yesu alitupa amri akisema katika Yohana 13:34, "Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo".
Yesu anatupenda sana, na kwa sababu hiyo alitufia msalabani ili sisi tuokolewe kutoka katika dhambi. Anataka na sisi kwa sisi tufanye vivyo hivyo, kwamba tupendane. Upendo una tabia zake, nazo zinakupa kutenda wema kila wakati ( soma 1 Wakoritho 13).
Katika toleo hili utaweza kuelewa zaidi upendo wa Yesu kwetu sisi wanadamu. Kupitia makala ya Simulizi kwa mfano utasimuliwa jinsi Yesu alivyokasirika kuona wanafunzi wake wakiwakataza watoto wasiende kwake. Unajua Yesu alifanya nini siku hiyo? Karibu usome! Na usisahau makala nyingine, vibonzo na michezo. Yote yatakupa uelewa zaidi juu ya upendo wa Mungu kwetu.
KARIBU KUNUNUA SOMA BIBLIA DUKANI KWA TSH. 500 TU.