Contact Us

Use the form on the right to contact us.

Or use the information below to contact our main office in Dar es Salaam or Arusha.

Main office:

P.o. box 12772 Dar Es Salaam, Tanzania

Phone: +255 786 197 412

E-mail: salesmanager.somabiblia@gmail.com

Publishing department

Postal address: P.o. Box 2696 Arusha, Tanzania

Phone: + 255 787392951

E-mail: publishing.somabiblia@gmail.com

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

Duka la Soma Biblia Arusha – eneo jipya

Habari kutoka Soma Biblia

Duka la Soma Biblia Arusha – eneo jipya

Anne Gihlemoen

Nafasi hii mpya itatusaidia kueneza huduma zetu
— Martin Mwaisumo, Branch Manager Arusha

Duka la zamani

Wakati wa Scripture Mission na Soma Biblia kuungana tarehe 1/1/2015, duka la vitabu la tawi la Arusha lilihamishwa kutoka eneo la Scripture Mission, Sakina, hadi eneo dogo, Arusha mjini. Viongozi walijua kwamba itakuwa kwa muda mfupi tu, kwa sababu duka lilikuwa dogo sana, na vitabu vya Soma Biblia ni vingi.

Hivyo sasa ni kwa furaha kubwa kwamba tunaweza kuwakaribisha wateja wetu wote kwenye duka jipya linalopatikana katika eneo la TFA (karibu na Nakumatt), Sokoine Road. Ni eneo ambalo hata wateja wanaotoka mbali hawatakuwa na shida kulitafuta.

Ofa maalumu!

Tarehe 21/11/2016

Biblia -10%

Tenzi -20% (nakala moja hadi kumii)

“Nafasi hii mpya itatusaidia kueneza huduma zetu,” Branch Manager Martin Mwaisumo anaeleza. Martin amekuwa akifanya kazi bila kusimama tangu alipopewa ufunguo wa duka mwanzoni mwa Novemba, ili kila kitu kiandaliwe vizuri kwa ufunguzi. Jumatatu tarehe 14/11 walianza kuuza katika duka jipya, lakini siku kuu ya ufunguzi itakuwa Jumatatu tarehe 21/11. “Tumewapa wachungaji na wainjilisti wanaoishi Arusha mjini mwaliko wa pekee kwa ajili ya siku hii, lakini kila mmoja anayetaka kushirikiana nasi tutamkaribisha kwa furaha. Tunataka duka lijae!” Martin anacheka. “Siku hii tunawapa wateja wetu ofa maalumu: tutatoa kipunguzo cha 10%  kwenye bei za Biblia (aina mbalimbali) na 20% kwenye bei ya Tenzi. Pia tutajaribu kuwa na chai kwa wateja wote. Utakuwa muda mzuri!”

Tunawapongeza Mwaisumo na timu yote ya tawi la Arusha kwa duka jipya! Na tunaomba Mungu awasaidie kuliendesha kwa lengo kuu la Soma Biblia ambalo ni kusambaza Injili ya Yesu Kristo.

Wafanyakazi wa duka la Soma Biblia. Martin Mwaisumo, Melania Joakim na Praygod Kimaro.

Wasiliana nasi:

Martin Mwaisumo, Branch Manager Namba ya simu: +255 687 666 020/+255 766 615 746 Barua pepe: arusha.somabiblia@gmail.com

MUDA WA KAZI:

Jumatatu-Ijuma: 2:30 asb-11:00 jioni Jumamos: 2:30 asb-8 mchana