Maisha Mazuri kwa Watoto
Hutoa msaada thabiti kwa sisi sote tunaowalea watoto. Upendo pasipo mashartini mbinu ya msingi, lakini pia kukaa pamoja kunakojenga, nidhamuna mbinu nyinginezo zinafafanuliwa kwa makini. Kila atakaye kuwapa watoto wake maisha yaliyo na maendeleo yenye afya, yampasa akisome.
Msingi wa Imani
Ni hazina kubwa kwa wote wanaotaka kufahamu ukweli wa Imani ya Kikristo. Kimeandikwa na profesa wa theolojia mwenye fokasi ya Kiinjili na kwa lengo la kumwezesha msomaji kushuhudia, Namjua yeye nimwaminiye! Ni kitabu cha lazima kwa kila aliye na huduma ya kufundisha kanisani.
Theolojia ya Martin Luther
Jifunze jinsi matengenezo ya Kanisa yalivyo na maana hadi sasa.
Imani ya Mtoto
Kinafafanua mtoto anavyotambua tofauti na mtu mzima. Chombo muhimu kwa wazazi na waalimu wote wanaowafundisha watoto imani ya Kikristo.
Historia ya Kibiblia
Kwa njia ya visa 111 vya Biblia, historia ya Mungu na wanadamu inasimuliwa kwa lugha rahisi. Kitabu kinafaa kama ‘Biblia ya wakipaimara’.
Yesu ni Msingi wa Wakristo
Masomo 21 kuhusu imani na maisha ya Kikristo yaliyoandaliwa kipekee kwa ajili ya mafundisho ya Ubatizo kwa watu wazima na Kipaimara.
Imani Yangu
Je, unataka imani yako iimarike, na maisha yako yampendeze Mungu? Pata mafundisho mepesi na yenye kina wakati mmoja. Kwa vijana pia!
Hekima Kutoka Katekisimo
Maswali na majibu 602 juu ya imani na maisha ya Kikristo. Yatakuwa na manufaa kwa watu wengi hasa wanafunzi wa neno la Mungu.
Ubatizo wa Kikristo
Kitabu hiki kinakupa majibu sahihi kuhusu Ubatizo. Kwa mfano: Ni sahihi kuwabatiza Watoto wadogo? Na Ubatizo wa maji ni tofauti na Ubatizo wa Roho?
Roho Mtakatifu
Kuna maoni mengi kuhusu Roho Mtakatifu na kazi yake maishani mwetu. Kama ukitaka kujikita katika ukweli wa Biblia, kitabu hiki kitakusaidia.
Onjeni Bwana alivyo mwema
Kitabu hiki ni msaada wa kushiriki sakramenti ya Chakula cha Bwana kwa manufaa zaidi. Maelezo ya aina tatu: rahisi, ya kibiblia na ya kitheolojia.
Msingi wa imani
Ukitaka ‘mafuta’ ya mafundisho ya profesa kuhusu imani ya Kikristo, soma kitabu hiki! Cha lazima kwa wachungaji na walimu wa imani.
Israeli Kwa Mtazamo wa Kikristo
Kwa mwongozo wa Biblia, mwandishi anampeleka msomaji katika taifa la Israeli alipojifunua Mungu katika historia yake na Yesu alipoishi.
Imani ya Kiinjili - katika Mazingira ya Kiafrika
Vitabu vya ETE (Elimu ya Theolojia kwa Enezi) vimesaidia Waafrika wengi. Msomaji atamfahamu zaidi Mungu Muumba na Mungu Mwokozi.