Contact Us

Use the form on the right to contact us.

Or use the information below to contact our main office in Dar es Salaam or Arusha.

Main office:

P.o. box 12772 Dar Es Salaam, Tanzania

Phone: +255 786 197 412

E-mail: salesmanager.somabiblia@gmail.com

Publishing department

Postal address: P.o. Box 2696 Arusha, Tanzania

Phone: + 255 787392951

E-mail: publishing.somabiblia@gmail.com

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

UWA podcast cover.jpg

URITHI WA ADAMU MICHEZO YA REDIO

20. Urithi 5

Cathbert Msemo

Sehemu hii ya mwisho inatufundisha juu ya kufukuka kwake Yesu na kupaa Mbinguni. Yesu amefufuka. Kaburi lake liko wazi. Wanafunzi wa Yesu walifurahi sana kumuona tena. Alikula pamoja nao, walizungumza pamoja, na aliwafundisha kwa jinsi ile ile kama ilivyokuwa kabla.Yesu, mkombozi wa ulimwengu, akapaa juu mbinguni kwa baba yake. Kazi aliyotumwa na Mungu wetu aliimaliza. Mpango wa Mungu kwawanaadamu umetimia. 

Urithi_Radio_20.jpg

 

19. Urithi 4

Cathbert Msemo

Yesu alisema: Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kristo ameuawa bila kosa, damu yake imemwagika msalabani bila hatia yoyote ameuawa na wanadamu. Sasa ni harakati za kwenda kuuzika mwili wake. Yosefu alikuwa amechongesha kaburi jipya kwa ajili yake mwenyewe karibu na Yesu aliposulubishwa. Basi, alinunua sanda nzuri akauviringishia mwili wa Yesu na kisha akauzika kaburini mwake, akaviringisha jiwe kubwa kuziba Kaburi lile. Nje Mariamu, mama yake Yesu na Mariamu Magdalena walisimama wakimsubiri kwa huzuni na majonzi tele. Iliwalazimu kuharakisha kwasababu kesho yake ni siku ya sabato, siku ambayo kwa sheria za wayahudi  wasingeweza kufanya kazi siku hiyo. Karibu kusikiliza kipindi hiki cha kusisimua

Urithi_Radio_19.jpg


18. Urithi 3

Anne Gihlemoen

Yesu hakuwa na hatia, lakini wamemkamata, wamemtesa na kumdhihaki. Yeye aliwaambia wale askari kuwa "huu ni wakati wenu hasa wakati wa utawala wa giza". Yesu anapelekwa kwa Pontio Pilato kupewa hukumu, wakati huo askari waliendelea kumtesa sana Bwana Yesu, walimpiga kwa mijeredi wakamvisha taji la miiba, wakamvisha joho jekundu, huku wakimtemea mate na kumkashifu sana. Yesu anazungushwa mitaani akiwa amebebeshwa msalaba mzito uliomuelemea hata ikalazimu simon wa mkirene kijana mkulima amsaidie kuubeba. Je, wanampeleka wapi sasa? Endelea kusikiliza sehemu hii

Urithi_Radio_18.jpg

16. Urithi 1

Anne Gihlemoen

Siku zimepita baada ya Bwana Yesu kuzaliwa. Naye aliendelea kukua katika hekima na kimo akimpendeza Mungu na wanadamu. Alipita sehemu zote za Israeli akifundisha neno la Mungu na kuponya wenye magonjwa. Habari ya miujiza ya Bwana Yesu ilienea kila mahali.

Read More

11. Mfalme 4

Cathbert Msemo

Muda wote Sauli alikuwa ndani ya Ikulu akitafakari jinsi wananchi wake walivyompokea Daudi mapokezi ambayo hata yeye tangu awe Mfalme hajawahi kupokewa hivyo...alimuangalia Daudi kwa jicho la chuki, hasira na kisasi. Daudi hakuwa amegundua chuki za mfalme Sauli juu yake. Alikuwa amesimama tu pembeni karibu na dirisha ndani ya ikulu ya Sauli akiongea na Yonathani. Mchezo huu wa Mfalme 4 unaeleza kwa undani.

Mfalme_Radio_11.jpg

10. Mfalme 3

Cathbert Msemo

Vitisho vya Goliath viliongezeka kila uchao. kila siku Goliath na jeshi lake la wafilisti walipanda mpaka Efes Damin na kuwatisha Sauli na wananchi wake.sauti yake ilitingisha nchi yote ya Israel. watu walikosa raha, Mfalme Sauli alikosa raha. Goliath alikuwa ni jitu la kutisha refu ajabu lenye miguu mikubwa ya ajabu mikono mikubwa kifua kilichojaa kama cha Simba dume. Sauti yake ilitisha kila alipoongea hata ndege kwenye miti waliruka kwa mstuko. Sikiliza kipindi hiki cha tatu usikie zaidi.

Mfalme_Radio_10.jpg

9. Mfalme 2

Cathbert Msemo

Mungu alimpa Daudi roho hivyo alipaswa kuwa na vifaa kwa kushughulikia kazi kama mfalme, wakati Mfalme Sauli maarufu alikuwa na kitu kingine tofauti kabisa, wakati huo huo Daudi akipokea roho, Roho wa Mungu akamwondoka Sauli. Mfalme Sauli alishikwa na ugonjwa wa ajabu akawa kama mtu aliyechanganyikiwa au aliye na mapepo. Kitu gani kinaendelea? Kipindi hiki cha Mfalme 2 kinaelezea vizuri zaidi.

Mfalme_Radio_09.jpg

8. Mfalme 1

Cathbert Msemo

Ilikuwa ni zaidi ya miaka elfu moja baada ya Mungu kumuahidi Abrahamu kwamba atakuwa baba wa mataifa mengi na kuwa mfalme atatoka katika ukoo wake, mkombozi wa ulimwengu. Ukoo wake umekuwa watu wenye nguvu wa asili ya Kiarabu na wana wa Israeli. Wana wa Israeli hawakuwa na Mfalme ambaye ameweza kuwakusanya wao kuwa taifa moja. Mungu akawapa Sauli. Je, mambo yalikuwaje? Sikiliza kipindi hiki.

Mfalme_Radio_08.jpg

1. Anguko la dhambi 1

Editor Soma Biblia

URITHI WA ADAMU ni mfululizo wa hadithi kutoka kitabu cha Biblia Takatifu. Katika sehemu ya kwanza tukiwasimulia mwanzo wa uummbaji wa ulimwengu, mwanadamu alivyoishi katika bustani ya Eden kwa furaha ya mahusiano yake na Mungu. Mmojawapo wa Malaika wa mbinguni, Shetani, alitaka kuchukua nafasi ya Mungu. Lakini hakuweza. Akafurushwa na kutupwa duniani kutoka mbinguni pamoja na wote waliomuunga mkono.

Read More