Soma Biblia
Maduka yanayotembea

Katika kuhakikisha vitabu vyetu vinamfikia kila mtu, tuna madereva ambao kila wiki wanajaza magari yao vitabu na Biblia kwenda kuuza vijijini. Wanaweka meza nje ya Makanisa baada ya ibada za jumapili, wanauza kwenye maduka madogomadogo ya vitabu au kusimama njiani na kuuza moja kwa moja wakiwa kwenye gari.

Kama unahitaji gari letu la vitabu kusimama na kuuza karibu na wewe,
tafadhali wasiliana na dereva aliyepo karibu nawe au agiza mzigo na utafikishiwa.

Madereva