Karibu Soma Biblia
Watoto wapendwa, karibuni! Katika toleo hili la Twende, tutajifunza kuhusu wanyama katika Biblia kama njiwa, punda na kondoo. Mungu aliwatumia kufundisha imani na maisha. Utapata michezo, vibonzo, mistari ya Biblia na wimbo wa sifa. Usikose zawadi kutoka Dada Rehema!
Nunua dukani Soma Biblia kwa 1000 tu.
“Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache” (Mt 9:37). Toleo hili la RIZIKI linakukaribisha kutafakari wito wa Yesu kwa kila muumini kushiriki katika shamba la Bwana. Usisubiri wengine, bali jiandae na ujitolee kuonesha upendo wa Kristo kwa vitendo. Karibu usome!
Soma kupitia HAPA
Kila mwanadamu amepewa zawadi ya maisha, lakini si wote hujiandaa kwa safari ya uzee. Biblia inafundisha: “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana” (Mhu 12:1). Toleo hili la RIZIKI linakukaribisha kutafakari kuzeeka kwa heshima, hekima na urithi wa kiroho. Karibu usome na ujifunze zaidi!
Unaweza kusoma bure kupitia HAPA
Toleo hili la Twende linakukaribisha kusoma na kutafakari zaidi juu ya upendo wa Mungu. Mungu hawezi kutuacha. Hatuachi gizani, anatupa tumaini jipya na furaha kila wakati. Karibu tusome pamoja, ujifunze kupitia makala, vibonzo na michezo, ukumbuke maisha ni salama kwa sababu Mungu hatuachi kamwe.
Nunua dukani Soma Biblia 1000 tu.
Ni furaha kuwaletea toleo hili la pili kwa mwaka 2025. Kwa lugha rahisi kabisa ndani ya toleo hili tutajifunza zaidi juu ya kumtumikia Mungu. Mtu mmoja alisema; "Mimi na nyumba yangu tutamtumikia Mungu". Je, wewe utamtumikia nani?
Karibu kununua katika maduka ya Soma Biblia.
Ni furaha kubwa kuwaletea wasomaji wa Riziki toleo hili la pili la mwaka 2025. Ujumbe wake ni kwamba Roho Mtakatifu ndiye mwalimu wetu mkuu.
Wasiliana nasi ukipenda kupokea kwa nia ya posta. Bonyeza Hapa
Katika maisha haya watu wengi wanatumia damu ya Yesu kwa mambo mengi. Lakini je, matumizi haya yote ni sawa? Soma toleo hili lenye kichwa ‘Neema Yatosha’.
Soma Riziki hapa Bure
Nikukaribishe kusoma toleo hili kuhusu Nuru ya Ulimwengu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hili. Usisahau michezo pamoja na katuni. Pia katika Sala ya Vijana utajifunza jinsi unavyoweza kuwa kielelezo kwa wengine ili nao wavutwe kumfuata Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Karibu tusome! Nunua dukani Soma Biblia kwa Shilingi 500 tu.
Bonyeza link kununua dukani Soma Biblia Dar es Salaam, Mbezi Luis, Arusha, Mbeya, Iringa, Mwanza
Ni sawa kabisa kuyaita majengo yetu makubwa na mazuri kanisa. Maana yake ni mahali pa kuabudia. Katika toleo hili tutaagalia maana nyingine ya Kanisa, herufi K ikiwa kubwa. Kanisa hili si jengo bali ni sisi tunaomwamini Yesu Kristo. Ndiyo maana tunasema, "Sisi ni Kanisa la Mungu".
Bonyeza link kununua dukani Soma Biblia Dar es Salaam, Mbezi Luis, Arusha, Mbeya, Iringa, Mwanza
Mada kuu katika toleo hili la nne la Riziki 2024 inasema, Katika bonde bado Mungu yupo? Ni swali ambalo ni muhimu kutafakari ili tuwatie moyo wale ambao wanapita katika hali ngumu na kukata tamaa. Ni msaada kwa wale ambao wanapita na watakaopita katika bonde la uvuli wa mauti na kuogopa kuwa hakuna tumaini tena kwa maisha ya mbele.
SOMA BIBLIA Society ni shirika la wahisani lisilo la kutengeneza faida wala kuwa na mwelekeo wa kisiasa. Lengo letu kuu ni kusambaza Injili ya Yesu Kristo kwa Kiswahili, kwa kuandaa Kanisa kupitia kuendeleza, kuzalisha na kusambaza Biblia kwa njia ya sauti, machapisho ya kuaminika juu ya Injili na vifaa vingine, vyote kwa Kiswahili. Shabaha nyingine ni kuwasaidia Wakristo kufikisha Injili kwa watu na kuwafundisha kupitia neno la Mungu – juu ya imani na maisha.
Idara ya Uchapishaji
Kama ukiwa na mswada au kutaka Soma Biblia kusambaza kitabu chako. Pia masuala ya Riziki, Twende, na Soma Biblia kwa Njia ya Mtandao
Simu: +255 787 392 951
Barua Pepe: publishingmanager.somabiblia@gmail.com
Anuani ya Posta: S.L.P. 2696, Arusha, Tanzania
Makao: Eneo la Sakina, upande wa pili wa sheli ya mafuta ya Oryx (kituo cha basi huitwa Oil Com). Fuata kibao cha Scripture Mission.
Idara ya Mauzo
Kama ukitafuta kitabu na bei yake, au kutaka kuagiza na kununua vitabu
Simu: +255 754 292 995
Baruapepe: manager.somabiblia@gmail.com
Anuani ya Posta: S.L.P. 12772, Dar es Salaam, Tanzania
Makao: Barabara ya Mwai Kibaki, Mikocheni B, upande wa pili wa Sanitas Medical Centre
Maduka yanapatikana Dar es Salaam (Mikocheni B & Mbezi Luis), Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma na Iringa