Contact Us

Use the form on the right to contact us.

Or use the information below to contact our main office in Dar es Salaam or Arusha.

Main office:

P.o. box 12772 Dar Es Salaam, Tanzania

Phone: +255 786 197 412

E-mail: salesmanager.somabiblia@gmail.com

Publishing department

Postal address: P.o. Box 2696 Arusha, Tanzania

Phone: + 255 787392951

E-mail: publishing.somabiblia@gmail.com

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

Peleka Injili kwa Vijana

Habari kutoka Soma Biblia

Peleka Injili kwa Vijana

Cathbert Msemo

Hodiiii! Tunawaletea vijana habari njema za Yesu Kristo.

Soma Biblia tuna mradi mpya wa kufikisha Injili kwa vijana kupitia kijitabu kinachoitwa Masiha. Kwa njia ya vibonzo, kijitabu hicho kinasimulia habari za Agano Jipya kuhusu maisha ya Yesu hapa duniani tangu kuzaliwa kwake mpaka alipopaa Mbinguni. Ni pamoja na mafundisho yake, na kusulubiwa, kufa na kufufuka kwake.

Wasambazaji wetu wamejipanga kutembea kwenye vipindi vya dini katika shule za msingi na sekondari ili kukutana na vijana na kuwagawia nakala ya Masiha. Lengo ni kuamsha ari ya vijana katika kujifunza maisha ya Yesu na kuishi katika imani kwake. 

Mathayo Massawe, Meneja wa mauzo wa Soma Biblia, na Simon, kijana ajitoaye kwa ajili ya mradi huu, walitembelea Shule ya Mbezi Juu na kuwakuta wanafunzi vijana wakiwa katika kipindi cha dini. Waliwagawia kijitabu cha Masiha. Wanafunzi walifurahi sana na kukipenda.

Mradi huu unaendelea Dar es Salaam na Arusha, tukilenga kutembelea baadhi ya shule za msingi na sekondari na kuwapa vijana kijitabu cha Masiha. Tunapenda kuwakaribisha wainjilisti na waalimu kanisani kuwa sehemu ya uinjilisti huu kwa vijana wengi ambao hawajamjua Yesu bado. Kama wewe unasimamia huduma mashuleni, unaweza kuwasiliana na tawi la Soma Biblia Arusha au Dar ili kutualika kutembelea shule unayohudumu. 

Bonyeza Arusha au Dar es Salaam kupata anuani za tawi husika