Contact Us

Use the form on the right to contact us.

Or use the information below to contact our main office in Dar es Salaam or Arusha.

Main office:

P.o. box 12772 Dar Es Salaam, Tanzania

Phone: +255 686 313 721 or +255 744 339 167

E-mail: manager.somabiblia@gmail.com

Publishing department

Postal address: P.o. Box 2696 Arusha, Tanzania

Phone: + 255 787392951

E-mail: publishingmanager.somabiblia@gmail.com

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

Riziki toleo 2/2025 'Linapatikana'

Habari kutoka Soma Biblia

Riziki toleo 2/2025 'Linapatikana'

Cathbert Msemo

ROHO MTAKATIFU MWALIMU WETU

Je, tunajifunza kutoka kwa nani?

Ni furaha kubwa kuwaletea wasomaji wa Riziki toleo hili la pili la mwaka 2025. Ujumbe wake ni kwamba Roho Mtakatifu ndiye mwalimu wetu mkuu.

Pengine umewahi kujiuliza jinsi Roho Mtakatifu anavyokuongoza kama mwalimu na msaidizi, kwa mfano wakati wa changamoto na majaribu? Na je, unampa nafasi ya ku­fanya hivyo katika maisha yako?

Makala ya mada kuu inatukumbusha jinsi tulivyo wa­sahaulifu wa mafundisho ya Yesu. Lakini inaonesha pia jinsi Roho Mtakatifu anavyotwaa katika yaliyo yake Yesu na kutupasha habari yake. Tunapomtegemea Mwalimu wetu, hatupotezi mwelekeo, bali tunapata nguvu mpya ya kupambana na changamoto za maisha.

Ulimwengu wa kidijitali ni mojawapo. Una ushawishi mkubwa kwetu siku hizi. Vijana wanakabiliwa na changa­moto nyingi katika masuala ya mahusiano na ndoa. Hata kama tuko wengi tunaotafuta kuwasaidia, swali hujitokeza: Nani aweze kuwapa kizazi cha kidijitali kujenga ndoa imara kwenye msingi wa uaminifu na maadili ya kikristo?

Makala ya Sasa sina woga wa kifo yatoa jibu. Anaye-shuhudia anasema, ”Neno la Mungu lilianza kunifungua macho na kunipa majibu yale yote ambayo nilikuwa ni­meyahangaikia kwa miaka mingi. Sasa kitabu hiki kinazungumza nami moja kwa moja.” Bila shaka sababu ni Roho Mtakatifu, mwalimu wetu!

Je, wimbo wa zamani unaweza kutusaidia hata leo? Tu­mechunguza Roho Mtakatifu Mungu Wetu ili kupata jibu. Wimbo huu unaonesha jinsi Roho Mtakatifu anavyohusika na yote tunayosikia ni muhimu kwa maisha yetu.

Kwa utangulizi huu mfupi nasema, Karibu kwenye Riziki!