Soma Biblia kwa Njia ya Mtandao

Huduma hii ni kwa wote wanaotaka kusoma vitabu vya Soma Biblia kwa manufaa zaidi, kwa kupata mwongozo, ushauri na mrejesho katika kujifunza.

Kozi yenye maswali

Vitabu vinaandaliwa kama kozi yenye maswali yanayokusaidia kuelewa ujumbe wa kitabu.

Mwalimu anakushauri

Majibu yako yatasahihishwa na utapokea maoni na maelezo ya kukusaidia zaidi.

Cheti cha mafanikio

Ukifaulu vizuri utapokea cheti cha kuthibitisha kuwa umesoma na kuelewa kitabu husika.

Mafunzo ni bure

Gharama ya kusoma ni bei ya kitabu tu.

JINSI YA KUJIUNGA
01

Chagua na nunua kitabu unachotaka kusoma.

02

Jaza fomu na uchague eneo ulipo pamoja na njia ya kusoma.

03

Utapokea maswali na kuyajibu kulingana na kitabu ulichosoma.

04

Majibu yatasahihishwa na utapokea mrejesho pamoja na cheti ukifaulu vizuri.

i
Unahitaji msaada?

Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi kuhusu kozi.

Jiunge na Kozi

Jaza taarifa zako hapa chini ili kuanza safari yako ya kujifunza.

🔒 Taarifa zako zitatumwa kwa Soma Biblia kwa ajili ya kushughulikiwa kwa usalama.

Mafanikio ya Kozi

Karibu ujiunge na ushirika wa kusoma Vitabu vya Kikristo kwa manufaa zaidi

📚
13
Vitabu na Kozi

Vitabu na kozi za Soma Biblia.

👨‍🎓
200
Wanafunzi

Idadi ya wanafunzi wanaojifunza kupitia mtandao.

✉️
100
Barua

Barua zenye maswali ya kutafakari na kujibu kwa kila kozi.

🎓
150
Wahitimu

Wanafunzi waliohitimisha kozi zote 13 na kupata vyeti.

Vitabu

Chagua kitabu unachopenda kuanza nacho na jiunge na kozi hiyo yenye mafundisho mazuri ili ukue katika imani na maisha ya Kikristo.

Onjeni Bwana Alivyo Mwema

Onjeni Bwana Alivyo Mwema

Philip Bach-Svendsen

Inafundisha maana ya Chakula cha Bwana/Ushirika Mtakatifu na umuhimu wake kwa anayeshiriki.

✉ Barua 5 📖 Biblia
Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu

Enok Sørensen

Mafundisho juu ya Roho Mtakatifu na kazi yake, ubatizo wa Roho na karama za Roho.

✉ Barua 14 📖 Mafundisho
Ubatizo wa Kikristo

Ubatizo wa Kikristo

Svend Aage Jacobsen

Inafafanua mafundisho ya Biblia juu ya ubatizo wa Kikristo kwa maneno ya Yesu.

✉ Barua 7 ✝ Imani
Israeli kwa Mtazamo wa Kikristo

Israeli kwa Mtazamo wa Kikristo

Samuel Roswall

Inafundisha maana ya Israeli kwa Mkristo na historia ya Biblia katika Israeli.

✉ Barua 3 📖 Historia
Historia ya Kibiblia

Historia ya Kibiblia

V. Vogt na J. Jossang

Inafundisha historia ya Agano la Kale kwa kifupi na kwa mtazamo wa Biblia.

✉ Barua 10 📜 Agano la Kale
Maombi

Maombi

Ole Hallesby

Inakusaidia kuelewa jinsi ya kuomba na nguvu iliyopo katika maombi.

✉ Barua 8 🙏 Maombi
Mwongozo kwa Familia ya Kikristo 1

Mwongozo kwa Familia ya Kikristo 1

Waandishi mbalimbali

Mafundisho na maelekezo ya Kibiblia juu ya familia ya Kikristo katika ulimwengu unaobadilika.

✉ Barua 10 👨‍👩‍👧 Familia
Mwongozo kwa Familia ya Kikristo 2

Mwongozo kwa Familia ya Kikristo 2

Waandishi mbalimbali

Makala 12 kuhusu maisha ya familia kwa mpango wa Mungu, matatizo ya vijana na mashauri mazuri.

📚 Makala 12 👨‍👩‍👧 Familia
Wokovu Maana na Matokeo

Wokovu Maana na Matokeo

David Ngassapa

Inafundisha wokovu ni nini na jinsi ya kuchagua njia ya kweli.

✉ Barua 5 ✝ Wokovu
Imani Yangu

Imani Yangu

Gudmund Vinskei

Inafundisha mambo makuu katika imani ya Kikristo kwa kifupi na kwa uelewa rahisi.

✉ Barua 10 ✝ Imani