Soma habari mpya kutoka Soma Biblia

Riziki 2/2026 - Mavuno ni mengi Watenda kazi wachache

“Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache” (Mt 9:37). Toleo hili la RIZIKI linakukaribisha kutafakari wito wa Yesu kwa kila muumini kushiriki katika shamba la Bwana. Usisubiri wengine, bali jiandae na ujitolee kuonesha upendo wa Kristo kwa vitendo. Karibu usome!

Soma kupitia HAPA

Read More

Riziki 1/2026 - Kuzeeka kwa heshima

Kila mwanadamu amepewa zawadi ya maisha, lakini si wote hujiandaa kwa safari ya uzee. Biblia inafundisha: “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana” (Mhu 12:1). Toleo hili la RIZIKI linakukaribisha kutafakari kuzeeka kwa heshima, hekima na urithi wa kiroho. Karibu usome na ujifunze zaidi!

Unaweza kusoma bure kupitia HAPA

Read More
Twende, Watoto, VIJANA Cathbert Msemo Twende, Watoto, VIJANA Cathbert Msemo

Twende 1/2026 - Mungu hawezi kuniacha

Toleo hili la Twende linakukaribisha kusoma na kutafakari zaidi juu ya upendo wa Mungu. Mungu hawezi kutuacha. Hatuachi gizani, anatupa tumaini jipya na furaha kila wakati. Karibu tusome pamoja, ujifunze kupitia makala, vibonzo na michezo, ukumbuke maisha ni salama kwa sababu Mungu hatuachi kamwe.

Nunua dukani Soma Biblia 1000 tu.

Read More
Magazeti, Twende, Watoto na Vijana Cathbert Msemo Magazeti, Twende, Watoto na Vijana Cathbert Msemo

Twende toleo la 1/2025 - 'Linapatikana'

Nikukaribishe kusoma toleo hili kuhusu Nuru ya Ulimwengu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hili. Usisahau michezo pamoja na katuni. Pia katika Sala ya Vijana utajifunza jinsi unavyoweza kuwa kielelezo kwa wengine ili nao wavutwe kumfuata Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Karibu tusome! Nunua dukani Soma Biblia kwa Shilingi 500 tu.

Bonyeza link kununua dukani Soma Biblia Dar es Salaam, Mbezi Luis, Arusha, Mbeya, Iringa, Mwanza

Read More
Twende, Watoto, Watoto na Vijana, Magazeti Cathbert Msemo Twende, Watoto, Watoto na Vijana, Magazeti Cathbert Msemo

Twende toleo la 4/2024 'linapatikana'

Ni sawa kabisa kuyaita majengo yetu makubwa na mazuri kanisa. Maana yake ni mahali pa kuabudia. Katika toleo hili tutaagalia maana nyingine ya Kanisa, herufi K ikiwa kubwa. Kanisa hili si jengo bali ni sisi tunaomwamini Yesu Kristo. Ndiyo maana tunasema, "Sisi ni Kanisa la Mungu".

Bonyeza link kununua dukani Soma Biblia Dar es Salaam, Mbezi Luis, Arusha, Mbeya, Iringa, Mwanza

Read More
Magazeti, RIZIKI, Zana za kusoma Biblia, Mahubiri Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI, Zana za kusoma Biblia, Mahubiri Cathbert Msemo

RIZIKI toleo la 4/2024 'linapatikana'

Mada kuu katika toleo hili la nne la Riziki 2024 inasema, Katika bonde bado Mungu yupo? Ni swali ambalo ni muhimu kutafakari ili tuwatie moyo wale ambao wanapita katika hali ngumu na kukata tamaa. Ni msaada kwa wale ambao wanapita na watakaopita katika bonde la uvuli wa mauti na kuogopa kuwa hakuna tumaini tena kwa maisha ya mbele.

Read More
Magazeti, Watoto, Watoto na Vijana, Twende Cathbert Msemo Magazeti, Watoto, Watoto na Vijana, Twende Cathbert Msemo

Twende Toleo la 4/2023 'linapatikana'

Nikukaribishe kusoma toleo hili. Linatufundisha kuwa sisi ni zawadi ya Mungu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hilo. Je, unamkumbuka mtoto aliyekuwa na kikapu chenye samaki wawili na mikate mitano? Soma uk.14 uone mtoto huyu alifanya nini akawa baraka ya Mungu kwa maelfu ya watu. Usisahau michezo na katuni kuhusu Dada Rehema na wadogo zake. Karibu Soma Biblia upate nakala kwa Tsh. 500 tu.

Read More
RIZIKI, Magazeti Cathbert Msemo RIZIKI, Magazeti Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO LA 4/2023 linatatikana 'Yesu kristo Ni njia ya uzima'

Mada kuu katika toleo hili la nne la Riziki 2023 ni Yesu Kristo ni njia ya uzima. Kuna njia nyingi,  lakini tunakumbushana kuwa kuna njia moja tu ya kumwingiza mtu katika furaha ya kweli ya milele. Kuna ukweli mmoja tu umfanyao mtu kuwa huru. Kuna namna moja tu ya maisha itakayomfikisha mtu katika uzima wa milele. Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ndiye Njia hiyo moja.

Read More