17. Urithi 2
Yesu anaendelea kufundisha na kufanya miujiza mikuu. Watu wengi wanamwamini na kumfuata. Ni wakati huu pia ambapo watawala walizidi kukasirika na kuamua kumkamata Yesu.
16. Urithi 1
Siku zimepita baada ya Bwana Yesu kuzaliwa. Naye aliendelea kukua katika hekima na kimo akimpendeza Mungu na wanadamu. Alipita sehemu zote za Israeli akifundisha neno la Mungu na kuponya wenye magonjwa. Habari ya miujiza ya Bwana Yesu ilienea kila mahali.
15. Mkuu wa Amani 4
Yesu akazaliwa! Sikiliza kipindi hiki kujua zaidi kuhusu wageni waajabu waliowatembelea Yusufu na Mariamu baada ya Yesu kuzaliwa.
14. Mkuu wa Amani 3
Yusufu na mkewe Mariamu walikuwa wanahangaika kutafuta mahali atakapozaliwa Mfalme mpya mwokozi wa ulimwengu ajaye kutimiza mpango wa Mungu.
13. Mkuu wa Amani 2
Zikiliza jinsi Yusufu alikuja kugundua ukweli juu ya mtoto Mariamu alikuwa akizaa, na jinsi walipaswa kukimbilia Bethlehemu ili kuhesabiwa na utawala wa Kirumi.
12. Mkuu wa Amani 1
Ni miaka elfu moja imepita tangu Mfalme Daudi alipofaulu kuwakusanya watu wa Israeli wawe kitu kimoja. Mungu alimuahidi Daudi kuwa ufalme wake utadumu hata milele, ila sasa hivi kuna shaka kama ahadi hii itatimizwa.
2. Anguko la dhambi 2
Shetani hakuwapenda kabisa Adamu na Eva. Basi akaweka mpango wa kuvunja upendo wa mwanadamu kwa Mungu.
1. Anguko la dhambi 1
URITHI WA ADAMU ni mfululizo wa hadithi kutoka kitabu cha Biblia Takatifu. Katika sehemu ya kwanza tukiwasimulia mwanzo wa uummbaji wa ulimwengu, mwanadamu alivyoishi katika bustani ya Eden kwa furaha ya mahusiano yake na Mungu. Mmojawapo wa Malaika wa mbinguni, Shetani, alitaka kuchukua nafasi ya Mungu. Lakini hakuweza. Akafurushwa na kutupwa duniani kutoka mbinguni pamoja na wote waliomuunga mkono.