RIZIKI TOLEO LA 2, 2020 'Sifa za Kiongozi Bora'

Wanaandaliwaje? 

Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna tunavyoweza kufikia maisha kwa kuandaa viongozi walio bora kuanzia katika umri wa ujana. Nia ni kuliamsha kanisa kama taasisi muhimu na ya kuaminika katika kuandaa viongozi wenye hofu ya Mungu, wenye maadili mema, wachapa kazi na walio tayari kuacha maslahi yao kwa ajili ya wengine.

Ndani ya toleo hili utakutana na kiongozi ambaye mfano wake unastahili kuigwa. Ingawa aliishi mbali na watu wake, alichukua hatua ya kuacha kazi yake nzuri ikulu na kwenda kuungana nao aliposikia habari za mateso yao. Hata upinzani haukumkatisha tamaa hadi alipofaulu kutekeleza mpango wake mzuri wa kuujenga upya mji wao ili wakae salama.

Pia utapata makala nyingine nzuri zinazoweza kuamsha ari ndani yako ya kuona umuhimu wa kuwaandaa viongozi vijana mapema kwa ajili ya kujenga kanisa na taifa kwa ujumla.

Soma Riziki Online HAPA

Previous
Previous

Twende toleo la 2/2020 linapatikana

Next
Next

TWENDE TOLEO 1, 2020 'Linapatikana'