Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
Peleka Injili kwa Vijana
Soma Biblia tuna mradi mpya wa kufikisha Injili kwa vijana kupitia kijitabu kinachoitwa Masiha. Kwa njia ya vibonzo, kijitabu hicho kinasimulia habari za Agano Jipya kuhusu maisha ya Yesu hapa duniani tangu kuzaliwa kwake mpaka alipopaa Mbinguni. Ni pamoja na mafundisho yake, na kusulubiwa, kufa na kufufuka kwake.