Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
YESU NI FIDIA - RIZIKI Toleo jipya
Yesu ni Fidia - kwa tafsiri rahisi neno fidia lina maana ya gharama ambayo inatolewa kwa ajili ya kufanya ukombozi. Yesu amelipa gharama yote kwa ajili yetu wanadamu. Hii ina maana gani hasa kwetu?
Kumbukumbu ya ”Mzee JJ”, Jon Jøssang 30.10.1926-30.12.2016
Kwa majonzi makubwa tunasikitika kutangaza kifo cha mwanzilishi wa Scripture Mission, Mzee Jon Jøssang. Mzee Jøssang amefariki tarehe 30 desemba, 2016 huko Norway alipokuwa akiishi na familia yake. Jøssang amefariki akiwa mzee wa umri wa miaka 90.