Twende 2/2026 - Wanyama katika Biblia
Cathbert Msemo
Mpendwa Msomaji
Watoto wapendwa, mnajua wanyama ni muhimu sana katika maisha yetu. Lakini hao sio tu rafiki zetu bali pia hutumiwa na Mungu katika kazi yake hapa ulimwenguni.
Je, mmeona jinsi wanyama walivyotumika sana katika Biblia kufundisha mambo ya imani na maisha? Kwa mfano kuna njiwa aliyemletea Nuhu tumaini baada ya gharika. Siku moja punda alimbeba Mfalme wa wafalme. Na punda mwingine alifanyika chombo cha ajabu; alizungumza kama sisi wanadamu. Hii ni ajabueee!
Katika toleo hili la Twende, tutaangalia baadhi ya wanyama katika Biblia na jinsi Mungu alivyowatumia kwa namna mbalimbali, ili tujifunze mambo mazuri kutoka kwao.
Utakutana na njiwa, nyati, punda, kondoo na wa-nyama wengine wengi. Bila shaka utapenda kumsifu Mungu ukiona wanavyoshuhudia ukuu wake. Kwa hiyo pia kuna wimbo wa sifa unaoweza kuuimba.
Na usisahau kufuatilia michezo, vibonzo na mistari mingine ya Biblia kuhusu wanyama ili ikupe hamu ya wewe kuendelea kuichunguza na kuijua Biblia yako. Kumbuka Dada Rehema ana zawadi kwa atakayejibu maswali na kuyatuma.
Na endapo una maswali, daima Kaka Kalamu yuko tayari kukujibu ukimwandikia. Karibu tusome!