Contact Us

Use the form on the right to contact us.

Or use the information below to contact our main office in Dar es Salaam or Arusha.

Main office:

P.o. box 12772 Dar Es Salaam, Tanzania

Phone: +255 686 313 721 or +255 744 339 167

E-mail: manager.somabiblia@gmail.com

Publishing department

Postal address: P.o. Box 2696 Arusha, Tanzania

Phone: + 255 787392951

E-mail: publishingmanager.somabiblia@gmail.com

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

Riziki 1/2026 - Kuzeeka  kwa heshima

Habari kutoka Soma Biblia

Riziki 1/2026 - Kuzeeka kwa heshima

Cathbert Msemo

Kuna haja ya kujiandaa kuzeeka?

Kila mwanadamu amepewa zawadi ya maisha, lakini siyo watu wote wanaofikia umri mkubwa au kujiandaa kwa safari ya kuzeeka. Biblia inatufundisha, “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya” (Mhu 12:1). Maneno haya yanatufundisha kuwa maandalizi ya uzee huanza mapema, katika ujana, kwa imani thabiti na nidhamu ya maisha.

Katika toleo hili la RIZIKI, tunatafakari maana ya kuzeeka kwa heshima. Kuzeeka siyo kupoteza thamani, bali ni hatua ya kuonesha hekima, urithi wa kiroho na heshima inayojengwa kwa muda mrefu. Tunajifunza kutoka kwa mifano ya watu wa Biblia kama Yakobo, ambaye uzee wake ulikuwa ushuhuda wa baraka na urithi wa imani.

Makala mbalimbali katika toleo hili zinatufundisha namna ya kuishi maisha yenye heshima na kujiandaa kwa uzee. Tutafakari kwa kina kuhusu kuzeeka kwa heshima, ushuhuda wa wazee wa imani, historia ya wimbo wa inji-li, pamoja na makala kuhusu familia na jamii. Yote haya yanatufundisha kuwa miili yetu ni hekalu la Mungu na maisha yetu ni ushuhuda wa baraka kwa vizazi vipya.

Huu ni mwaliko kwa kila msomaji kujiandaa kuzeeka kwa heshima, ili uzee wetu uwe ushuhuda wa imani, hekima na urithi wa kiroho unaoendelea kuangaza jamii na kanisa.