Twende toleo la 2/2025

Mimi nitamtumikia Bwana

Je, umewahi kusikia mtu akisema, "Mimi ni mtumi­shi wa umma" au "Mimi ni mtumishi wa taasisi"? Hawa ni watu wanaofanya kazi kwa maagizo ya mwajiri wao, wakileta faida na mabadiliko kwa jamii.

Lakini mtu anaposema, "Mimi ni mtumishi wa Mungu", anamaanisha nini? Je, Mungu amemwa­jiri? Hapana!

Kumtumikia Mungu ni kumfuata Yesu na kutenda yale anayopenda ili kuonyesha utukufu wake. Siyo kufanya kazi nyingi kwa kutafuta faida, bali ni ku­fuata maagizo yake na kutumia vipawa tulivyopewa na Mungu kwa njia inayompendeza.

Baadhi wanapenda kuimba, wengine kusaidia wenzao, wengine tena kufanya kazi fulani au ku­fundisha Neno la Mungu. Tunamtumikia Mungu kwa uaminifu na kwa moyo wa upendo, tukifanya mema kwa wengine.

Kwa lugha rahisi kabisa ndani ya toleo hili tutaji­funza zaidi juu ya kumtumikia Mungu. Mtu mmoja alisema; "Mimi na nyumba yangu tutamtumikia Mungu". Je, wewe utamtumikia nani?

Tutakuwa na vibonzo na michezo. Utasoma pia hadithi ya watoto walioanzisha wazo la kujenga nyumba ya mchungaji kanisani kwao na waka-fanikiwa wazo hilo. Huu ni utumishi wa mfano, sivyo! Karibu usome!

Nunua Soma Biblia Dukani

Previous
Previous

Twende 1/2026 - Mungu hawezi kuniacha

Next
Next

Riziki toleo 2/2025 'Linapatikana'