Soma habari mpya kutoka Soma Biblia

Twende, Watoto, VIJANA Cathbert Msemo Twende, Watoto, VIJANA Cathbert Msemo

Twende 1/2026 - Mungu hawezi kuniacha

Toleo hili la Twende linakukaribisha kusoma na kutafakari zaidi juu ya upendo wa Mungu. Mungu hawezi kutuacha. Hatuachi gizani, anatupa tumaini jipya na furaha kila wakati. Karibu tusome pamoja, ujifunze kupitia makala, vibonzo na michezo, ukumbuke maisha ni salama kwa sababu Mungu hatuachi kamwe.

Nunua dukani Soma Biblia 1000 tu.

Read More
Twende, Watoto, Watoto na Vijana, Magazeti Cathbert Msemo Twende, Watoto, Watoto na Vijana, Magazeti Cathbert Msemo

Twende toleo la 4/2024 'linapatikana'

Ni sawa kabisa kuyaita majengo yetu makubwa na mazuri kanisa. Maana yake ni mahali pa kuabudia. Katika toleo hili tutaagalia maana nyingine ya Kanisa, herufi K ikiwa kubwa. Kanisa hili si jengo bali ni sisi tunaomwamini Yesu Kristo. Ndiyo maana tunasema, "Sisi ni Kanisa la Mungu".

Bonyeza link kununua dukani Soma Biblia Dar es Salaam, Mbezi Luis, Arusha, Mbeya, Iringa, Mwanza

Read More
Magazeti, Watoto, Watoto na Vijana, Twende Cathbert Msemo Magazeti, Watoto, Watoto na Vijana, Twende Cathbert Msemo

Twende Toleo la 4/2023 'linapatikana'

Nikukaribishe kusoma toleo hili. Linatufundisha kuwa sisi ni zawadi ya Mungu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hilo. Je, unamkumbuka mtoto aliyekuwa na kikapu chenye samaki wawili na mikate mitano? Soma uk.14 uone mtoto huyu alifanya nini akawa baraka ya Mungu kwa maelfu ya watu. Usisahau michezo na katuni kuhusu Dada Rehema na wadogo zake. Karibu Soma Biblia upate nakala kwa Tsh. 500 tu.

Read More
Watoto, Watoto na Vijana Cathbert Msemo Watoto, Watoto na Vijana Cathbert Msemo

OFA SIKUKUU YA WATOTO 2023

Soma Biblia tunapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Tuko tayari kuchangia ili furaha na baraka ya sikukuu ya watoto iendelee muda mrefu. Inawezekana ikiwa watoto wanapewa zawadi ya kudumu zaidi ya chakula kizuri. Kwa hiyo tunatoa ofa maalumu ya vitabu fulani vinavyowafaa watoto pamoja na walezi wao wote wanaowafundisha imani na maisha ya Kikristo. Tazama picha kuona vitabu na bei ya punguzo

Read More
Magazeti, RIZIKI, Watoto, Watoto na Vijana Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI, Watoto, Watoto na Vijana Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO 03/2023 - Linapatikana

Je, mahubiri ya siku ya Siku Kuu ya Watoto  yanawalenga akina nani hasa? Ni kwa ajili ya wazazi wanaowalea watoto au ni kwa ajili ya watoto ambao kimsingi ndio wenye siku yao? Mada kuu ya toleo la tatu la Riziki inasema “tuwafundishe watoto wetu“. Lengo la mada hii ni kukumbushana kama familia, kanisa na jamii kuweka mkazo katika malezi ya watoto. “Na watoto wako wote watafundishwa na BWANA; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi” ( Isa 54:13). Karibu kusoma RIZIKI ONLINE BURE. BOFYA HAPA

Read More
Watoto, Magazeti, Twende Cathbert Msemo Watoto, Magazeti, Twende Cathbert Msemo

TWENDE TOLEO LA #03/2021 'Linapatikana'

Katika toleo hili la Twende tutajifunza zaidi kuhusu agano letu na Mungu. Ndiyo, hata sisi tunaweza kufanya agano na Mungu. Ubatizo wa Kikristo ni agano la aina hii. Vilevile utasoma kuhusu watoto waliomwahidi Mungu jambo fulani. Kama una swali kuhusu agano, karibu kumwandikia Kaka Kalamu. Yuko tayari kujibu, mia kwa mia! Karibu kununua katika maduka ya Soma Biblia kwa Tsh. 500/= tu.

Read More
Watoto, Ofa maalum Cathbert Msemo Watoto, Ofa maalum Cathbert Msemo

SIKUKUU YA WATOTO 2021

Sisi wa Soma Biblia tunapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Tuko tayari kuchangia ili furaha na baraka ya sikukuu ya watoto iendelee muda mrefu. Inawezekana ikiwa watoto wanapewa zawadi ya kudumu zaidi ya chakula kizuri. Kwa hiyo tunatoa ofa maalumu ya vitabu fulani vinavyowafaa watoto pamoja na walezi wao wote wanaowafundisha imani na maisha ya Kikristo.

Read More
Twende, Watoto, Magazeti Cathbert Msemo Twende, Watoto, Magazeti Cathbert Msemo

Twende Toleo la #4, 2020 linapatikana

Karibu kununua TWENDE kwa Tsh. 500 tu katika maduka ya Soma Biblia. Toleo hili linafafanua juu ya Uhusiano wetu na Mungu. Kwa njia ya simulizi na hadithi nzuri utaweza kuelewa juu ya jambo hili. Utakutana pia na Dada Rehema na wenzake, na kuna michezo ya kuvutia. Usisahau kututumia majibu yako kama ilivyoelekezwa kwenye uk.5 na nyuma ya gazeti.

Read More
Ofa maalum, Watoto Cathbert Msemo Ofa maalum, Watoto Cathbert Msemo

SIKU KUU YA WATOTO 2020

Sisi wa Soma Biblia tunapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Tuko tayari kuchangia ili furaha na baraka ya sikukuu ya watoto iendelee muda mrefu. Inawezekana ikiwa watoto wanapewa zawadi ya kudumu zaidi ya chakula kizuri.

Kwa hiyo tunatoa ofa maalumu ya vitabu fulani vinavyowafaa watoto pamoja na walezi wao wote wanaowafundisha imani na maisha ya Kikristo.

Read More