Soma habari mpya kutoka Soma Biblia

Magazeti, Twende Cathbert Msemo Magazeti, Twende Cathbert Msemo

Twende toleo #2/2022

Katika toleo hili tunajifunza juu ya 'Kukaza Mwendo'. Kupitia makala mbalimbali tutajifunza maana hasa ya kukaza mwendo kwenda Mbinguni, na zaidi tuta-elewa kuwa sisi ni washindi tunaoweza kuzishinda changamoto za dunia hii kwa sababu yupo mmoja ambaye anatuwezesha kushinda tukiwa naye.

Kuna kibonzo kitakachokufurahisha na kukufundisha kukaza mwendo bila kukata tamaa hadi kufikia ushindi. Usisahau dada Rehema! Ana michezo na ukijibu maswali vizuri unapata zawadi. Pia Kaka Kalamu anakukumbusha kumwandikia kama una swali, naye atakujibu. Karibu tusome!

Read More
RIZIKI Cathbert Msemo RIZIKI Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO LA 1, 2019 - 'Ukristo ni utamaduni au imani?'

Katika toleo hili la RIZIKI tunachunguza kama Ukristo ni imani au utamaduni. Nia ni kukumbushana kuwa, mapokeo ya dini yanaweza kuwa mazoea au taratibu tupu zisizo na faida. Kama mwandishi mmoja alivyoandika, ndivyo taratibu zilivyo kama misingi yake haikujengwa katika Kristo. Lakini vilevile tamaduni na mapokeo zitafaa, tena zitakuwa na faida, kama zinatuelekeza kumwamini Yesu na kufanya mapenzi yake. Karibu usome toleo hili

Read More