Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
Twende 1/2026 - Mungu hawezi kuniacha
Toleo hili la Twende linakukaribisha kusoma na kutafakari zaidi juu ya upendo wa Mungu. Mungu hawezi kutuacha. Hatuachi gizani, anatupa tumaini jipya na furaha kila wakati. Karibu tusome pamoja, ujifunze kupitia makala, vibonzo na michezo, ukumbuke maisha ni salama kwa sababu Mungu hatuachi kamwe.
Nunua dukani Soma Biblia 1000 tu.
RIZIKI TOLEO LA 1, 2020 'Ujenzi wa Familia Imara'
Katika toleo hili la RIZIKI tunaangalia mada isemayo, “Ujenzi wa familia imara”. Lengo ni kuibua na kujadili changamoto zilizopo kwenye taasisi hii muhimu ambayo mwanzilishi wake ni Mungu mwenyewe pale bustani ya Edeni. Ni wito wa kuliamsha kanisa na jamii yote, kuwa taasisi hii inapaswa kulindwa, kuimarishwa na kupiganiwa kwa nguvu zote.