Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
FIKIA MAISHA
Mambo vipi! Vijana, angalieni hapa, tumepata kifaa. Soma Biblia pamoja na Biblica Kenya tumezindua programu mpya ya vijana ijulikanayo kama FIKIA MAISHA. Sasa mambo ni poa kabisa.
Injili inawafikia vijana Arusha
Mradi mpya wa kupeleka habari njema ya Yesu Kristo kwa vijana wanaokaa Arusha umeanza. Soma Biblia tumetembelea Shule ya Sekondari Sombetini na kuwagawia wanafunzi karibu na 1500 nakala ya kijitabu cha Masiha. Wote walipenda kupata zawadi hii.
RIZIKI TOLEO LA 3, 2019 'TUNATAMBUAJE NAFASI YA WATOTO NA VIJANA NDANI YA KANISA?'
Je, wewe ni mtumishi wa Kanisa? Riziki toleo la Tatu mwaka 2019 linapatikana sasa.
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna ya kutambua nafasi ya watoto na vijana ndani ya kanisa. Nia ni kukumbushana kama kanisa umuhimu wa kuwatambua, ili tuwalee vizuri na kuwajali pamoja na vipaji walivyo navyo.