Injili inawafikia vijana Arusha

Mradi mpya wa kupeleka habari njema ya Yesu Kristo kwa vijana wanaokaa Arusha umeanza. Soma Biblia tumetembelea Shule ya Sekondari Sombetini na kuwagawia wanafunzi karibu na 1500 nakala ya kijitabu cha Masiha. Wote walipenda kupata zawadi hii. 

Ni mpango kutembelea shule hii tena siku ya kipindi chao cha dini. Tunapenda kujua jinsi wanafunzi walivyopokea ujumbe wa kitabu hiki, na kusaidiana na walimu wao kujibu maswali kama yamejitokeza wakati wa kusoma kuhusu kuzaliwa, kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo. 

Tunawakaribisha wote wanaosoma habari hii wajiunge nasi katika maombi kwamba kitabu hiki kitawasaidia wengi katika kumjua Mungu wa kweli na kumtegemea yeye. 

2020-02-27 12.09.28.jpg
2020-02-27 12.11.23.jpg
Previous
Previous

RIZIKI TOLEO LA 1, 2020 'Ujenzi wa Familia Imara'

Next
Next

Peleka Injili kwa Vijana