Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
RIZIKI toleo la 1/2025 'Linapatikana'
Katika maisha haya watu wengi wanatumia damu ya Yesu kwa mambo mengi. Lakini je, matumizi haya yote ni sawa? Soma toleo hili lenye kichwa ‘Neema Yatosha’.
Soma Riziki hapa Bure
Twende toleo 2/2024 'Linapatikana'
Karibu kusoma toleo hili ujifunze zaidi juu ya Yesu rafiki yetu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hili. Tsh. 500 tu.
Twende toleo 1/2024 'linapatikana'
Mfalme anaweza kuwa mzuri au mbaya. Akiwa mfalme mzuri anaonyesha upendo kwa watu wake, na hukumu zake ni za haki. Mfalme mbaya anafikiri juu ya maendeleo yake tu, na hana rehema kwa watu wake. Karibu kusoma toleo hili ujifunze zaidi juu ya Yesu, Mfalme wa wafalme.
TWENDE 2/2023 - Linapatikana
Katika toleo hili utaweza kuelewa zaidi upendo wa Yesu kwetu sisi wanadamu. Kupitia makala ya Simulizi kwa mfano utasimuliwa jinsi Yesu alivyokasirika kuona wanafunzi wake wakiwakataza watoto wasiende kwake. Unajua Yesu alifanya nini siku hiyo? Karibu usome! Na usisahau makala nyingine, vibonzo na michezo. Yote yatakupa uelewa zaidi juu ya upendo wa Mungu kwetu.
Bonyeza hapa kupata orodha ya bei ya vitabu mbali mbali na Biblia
RIZIKI TOLEO 4/2019 linapatikana "JE! YESU AMEPOTEA NJIA?"
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili kurudi kwa Yesu kama alivyoahidi. Lengo ni kusaidiana kama kanisa kupeana maarifa yenye uhakika juu ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Malengo ni wazi: Kwanza, tuwe na mafundisho sahihi kuhusu kurudi kwa Yesu. Pili, tuepukane na mafundisho ya uongo kuhusu jambo hili. Na tatu, tusije tukakata tamaa kuwa Kristo harudi, kisha tukalegea katika kuitenda kazi ya Mungu.
TWENDE TOLEO LA 4/2019 Linapatikana
Mtoto mwenzangu, toleo hili lina habari njema kuhusu maisha yetu ya sasa na ya baadaye. Tutambue kwamba tukiwa ndani ya Yesu tutakuwa salama sasa na siku zijazo, na hata tukifa tutaenda kuishi na Yesu kwa furaha mbinguni.
TWENDE TOLEO LA 2, 2019 Linapatikana
Umewahi kusikia mtu akisema, “Mimi ni mwanafunzi wa Yesu”? Au, “Mimi ni mtoto wa Yesu? Au, “Mimi ni mtumishi wa Yesu? Je, ana maana gani hasa? Soma makala za gazeti hili upate ufafanuzi mzuri kuhusu swali hili.
TWENDE TOLEO LA 1, 2019 Linapatikana
Karibu usome gazeti hili linalofafanua kuhusu safari yetu ya kwenda mbinguni. Linauzwa katika Maduka yote ya Soma Biblia na kwa dereva wetu wa mauzo anayezunguka na gari la kuuza vitabu na Biblia. Ni bei poa kabisa