RIZIKI TOLEO 4/2019 linapatikana "JE! YESU AMEPOTEA NJIA?"

Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? 

Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili kurudi kwa Yesu kama alivyoahidi. Lengo ni kusaidiana kama kanisa kupeana maarifa yenye uhakika juu ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Malengo ni wazi: Kwanza, tuwe na mafundisho sahihi kuhusu kurudi kwa Yesu. Pili, tuepukane na mafundisho ya uongo kuhusu jambo hili. Na tatu, tusije tukakata tamaa kuwa Kristo harudi, kisha tukalegea katika kuitenda kazi ya Mungu. 

Ndani ya toleo hili utakutana na kijana aliyezaliwa katika hali ya umaskini, lakini leo ni mashuhuri na ndiye mwanzo wa Ukristo wetu. Pia utakutana na maswali ya changamoto juu ya kurudi kwa Yesu. Yatakupa nafasi ya kujitafakari, ili ujiandae na kuwa na uhakika wa kwenda pamoja naye pale Kristo ajapo. Karibu usome kwa undani habari hizi.

Ukipenda kupokea kila toleo la RIZIKI bure kwa njia ya posta au ya barua pepe, jiunga kwa kuweka comment hapo chini au kutuandikia kwa njia ya barua pepe:  editor.somabiblia@gmail.com

Pia unaweza kusoma RIZIKI ONLINE kwa kubonjeza HAPA

Previous
Previous

NDOA YENYE FURAHA

Next
Next

TWENDE TOLEO LA 4/2019 Linapatikana