Soma habari mpya kutoka Soma Biblia

Magazeti, Watoto, Watoto na Vijana, Twende Cathbert Msemo Magazeti, Watoto, Watoto na Vijana, Twende Cathbert Msemo

Twende Toleo la 4/2023 'linapatikana'

Nikukaribishe kusoma toleo hili. Linatufundisha kuwa sisi ni zawadi ya Mungu. Makala zote zinafafanua vizuri jambo hilo. Je, unamkumbuka mtoto aliyekuwa na kikapu chenye samaki wawili na mikate mitano? Soma uk.14 uone mtoto huyu alifanya nini akawa baraka ya Mungu kwa maelfu ya watu. Usisahau michezo na katuni kuhusu Dada Rehema na wadogo zake. Karibu Soma Biblia upate nakala kwa Tsh. 500 tu.

Read More
Ofa maalum, Watoto Cathbert Msemo Ofa maalum, Watoto Cathbert Msemo

SIKU KUU YA WATOTO 2020

Sisi wa Soma Biblia tunapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Tuko tayari kuchangia ili furaha na baraka ya sikukuu ya watoto iendelee muda mrefu. Inawezekana ikiwa watoto wanapewa zawadi ya kudumu zaidi ya chakula kizuri.

Kwa hiyo tunatoa ofa maalumu ya vitabu fulani vinavyowafaa watoto pamoja na walezi wao wote wanaowafundisha imani na maisha ya Kikristo.

Read More
Watoto na Vijana Cathbert Msemo Watoto na Vijana Cathbert Msemo

SIKU KUU YA MIKAELI NA WATOTO IMEKARIBIA

Ni furaha yetu kuona jinsi Kanisa linavyoweka siku kuu ya pekee kwa ajili ya watoto. Soma Biblia tunapenda kushiriki katika kazi ya kuwajenga watoto katika imani ya Kikristo kwa njia ya vitabu, Biblia na majarida kwa ajili ya watoto. Kwa hiyo tunatoa ofa maalum kwa sharika zote zinazopenda kuwapa watoto wao zawadi kwaajili ya siku kuu ya watoto.  

Read More