Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
Riziki 2/2026 - Mavuno ni mengi Watenda kazi wachache
“Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache” (Mt 9:37). Toleo hili la RIZIKI linakukaribisha kutafakari wito wa Yesu kwa kila muumini kushiriki katika shamba la Bwana. Usisubiri wengine, bali jiandae na ujitolee kuonesha upendo wa Kristo kwa vitendo. Karibu usome!
Soma kupitia HAPA
Riziki 1/2026 - Kuzeeka kwa heshima
Kila mwanadamu amepewa zawadi ya maisha, lakini si wote hujiandaa kwa safari ya uzee. Biblia inafundisha: “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana” (Mhu 12:1). Toleo hili la RIZIKI linakukaribisha kutafakari kuzeeka kwa heshima, hekima na urithi wa kiroho. Karibu usome na ujifunze zaidi!
Unaweza kusoma bure kupitia HAPA