Ushuhuda wa Melania Joakim 'Yesu alinichagua bila gharama yoyote'

Yesu amenichagua mimi
Melania Joakim & Vivi Agerbo Joergensen
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni

Karibu kusikiliza ushuhuda wa Melania Joakim kuhusu jinsi alivyopata neema ya kumjua Mungu. Alijiunga tu nawenzake kwenda Shule ya Jumapili wakati akiwa mdogo. Pamoja na kwamba wazazi wake hawakuwa wakristo, hakukatazwa kuendelea kwenda Kanisani. Kupitia yeye sasa mama yake amashampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuna mengi ya kujifunza katika ushuhuda wake. Alifunuliwa habari za upendo mkuu wa Yesu aliposoma Yohana 15:16, Yaani Mungu ametuchagua bila gharama yoyote? Ni neema ya ajabu sana. Melania ni mfanyakazi wa Soma Biblia kwa miaka mitano sasa.

Melania Joachim 2 (2).jpg
Previous
Previous

Maisha ya Ebenezer Nelson Shafuri 'Mtu asiudharau Ujana wako'

Next
Next

Ushuhuda wa Letesi Chuma 'Kweli Mungu Yupo'