Twende Toleo la #4, 2020 linapatikana

MPENDWA MSOMAJI 

Ukiwa na rafiki, mnapendana, sivyo! Pia mnasaidiana, mmoja wenu akiwa na uhitaji. Watu wanapowaangalieni mkicheza pamoja, kwenda kanisani pamoja na kufanya mambo mengine mazuri pamoja, wanasemaje? Bila shaka wanaona mna mahusiano mazuri. 

Gazeti hili linahusu uhusiano wetu na Mungu. Najua unajiuliza, Uhusiano huu ukoje? 

Katika toleo hili la TWENDE tumefafanua mengi juu ya jambo hili kwa njia ya simulizi na hadithi nzuri. Utakutana pia na Dada Rehema na wenzake, na kuna michezo ya kuvutia. Usisahau kututumia majibu yako kama ilivyoelekezwa kwenye uk.5 na nyuma ya gazeti.

Karibu usome kwa Tsh 500.

Previous
Previous

RIZIKI TOLEO #4/2020 'Utupe leo riziki yetu'

Next
Next

Kalenda ya Ukutani 2021 inapatikana