Soma habari mpya kutoka Soma Biblia

Watoto, Watoto na Vijana Cathbert Msemo Watoto, Watoto na Vijana Cathbert Msemo

OFA SIKUKUU YA WATOTO 2023

Soma Biblia tunapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Tuko tayari kuchangia ili furaha na baraka ya sikukuu ya watoto iendelee muda mrefu. Inawezekana ikiwa watoto wanapewa zawadi ya kudumu zaidi ya chakula kizuri. Kwa hiyo tunatoa ofa maalumu ya vitabu fulani vinavyowafaa watoto pamoja na walezi wao wote wanaowafundisha imani na maisha ya Kikristo. Tazama picha kuona vitabu na bei ya punguzo

Read More
Twende, Watoto na Vijana, Magazeti Cathbert Msemo Twende, Watoto na Vijana, Magazeti Cathbert Msemo

TWENDE 2/2023 - Linapatikana

Katika toleo hili utaweza kuelewa zaidi upendo wa Yesu kwetu sisi wanadamu. Kupitia makala ya Simulizi kwa mfano utasimuliwa jinsi Yesu alivyokasirika kuona wanafunzi wake wakiwakataza watoto wasiende kwake. Unajua Yesu alifanya nini siku hiyo? Karibu usome! Na usisahau makala nyingine, vibonzo na michezo. Yote yatakupa uelewa zaidi juu ya upendo wa Mungu kwetu.

Bonyeza hapa kupata orodha ya bei ya vitabu mbali mbali na Biblia

Read More
Magazeti, Twende Cathbert Msemo Magazeti, Twende Cathbert Msemo

Twende toleo #2/2022

Katika toleo hili tunajifunza juu ya 'Kukaza Mwendo'. Kupitia makala mbalimbali tutajifunza maana hasa ya kukaza mwendo kwenda Mbinguni, na zaidi tuta-elewa kuwa sisi ni washindi tunaoweza kuzishinda changamoto za dunia hii kwa sababu yupo mmoja ambaye anatuwezesha kushinda tukiwa naye.

Kuna kibonzo kitakachokufurahisha na kukufundisha kukaza mwendo bila kukata tamaa hadi kufikia ushindi. Usisahau dada Rehema! Ana michezo na ukijibu maswali vizuri unapata zawadi. Pia Kaka Kalamu anakukumbusha kumwandikia kama una swali, naye atakujibu. Karibu tusome!

Read More
Watoto, Magazeti, Twende Cathbert Msemo Watoto, Magazeti, Twende Cathbert Msemo

TWENDE TOLEO LA #03/2021 'Linapatikana'

Katika toleo hili la Twende tutajifunza zaidi kuhusu agano letu na Mungu. Ndiyo, hata sisi tunaweza kufanya agano na Mungu. Ubatizo wa Kikristo ni agano la aina hii. Vilevile utasoma kuhusu watoto waliomwahidi Mungu jambo fulani. Kama una swali kuhusu agano, karibu kumwandikia Kaka Kalamu. Yuko tayari kujibu, mia kwa mia! Karibu kununua katika maduka ya Soma Biblia kwa Tsh. 500/= tu.

Read More
Twende, Watoto, Magazeti Cathbert Msemo Twende, Watoto, Magazeti Cathbert Msemo

Twende Toleo la #4, 2020 linapatikana

Karibu kununua TWENDE kwa Tsh. 500 tu katika maduka ya Soma Biblia. Toleo hili linafafanua juu ya Uhusiano wetu na Mungu. Kwa njia ya simulizi na hadithi nzuri utaweza kuelewa juu ya jambo hili. Utakutana pia na Dada Rehema na wenzake, na kuna michezo ya kuvutia. Usisahau kututumia majibu yako kama ilivyoelekezwa kwenye uk.5 na nyuma ya gazeti.

Read More
Magazeti Cathbert Msemo Magazeti Cathbert Msemo

Twende toleo no. 3, 2018 linapatikana sasa

Mpendwa msomaji wa Twende, uvumilivu ni tunda la Roho tunayepewa tunapomwamini Yesu. Biblia inatufundisha uvumilivu kupitia watu mbalimbali. Toleo hili limefafanua zaidi maana ya uvumilivu kwetu sisi Wakristo. Jipatie nakala yako kutoka Soma Biblia.

Read More