Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
Twende toleo no. 3, 2018 linapatikana sasa
Mpendwa msomaji wa Twende, uvumilivu ni tunda la Roho tunayepewa tunapomwamini Yesu. Biblia inatufundisha uvumilivu kupitia watu mbalimbali. Toleo hili limefafanua zaidi maana ya uvumilivu kwetu sisi Wakristo. Jipatie nakala yako kutoka Soma Biblia.
Namwamini Yesu Kristo - RIZIKI toleo la 3 2018
Toleo hili la RIZIKI tunaangalia sehemu ya pili ya Imani ya Mitume; Namwamini Yesu Kristo. Tunakumbushana kwa kutafakari maana ya maneno haya. Tunapokiri kwamba namwamini yesu, ina maana maisha yetu yamejengeka ndani ya msingi ambao ni Yesu Kristo.
"Imani ijaribiwapo" - RIZIKI toleo #3, 2017
Mimi na wewe tunaweza kuwa na maswali mengi yanayosumbua imani yetu kututilia wasiwasi mwingi wa kiroho.
"Majina ya Mungu", RIZIKI toleo la tatu
Majina ya Mungu yametumika ndani ya Biblia kama mwongozo wa kujifunza tabia ya Mungu. Toleo hili la RIZIKI linaeleza zaidi.