Kupendwa na Mungu - Wanawake wa Imani Kip #1
Je, umezingatia kwamba sisi wanawake tunacho kitu kama sanduku mioyoni mwetu. Sehemu inayopaswa kujaa upendo. Ni jinsi Mungu alivyotuumba. Lakini mara nyingi ninasikia utupu hapo, au tuseme nina kiu. Kiu ya kupendwa. Ebu fikiria ungeambiwa maneno matamu haya: “mna thamani mbele yangu, kwa kuwa nimewapa hadhi na kuwapenda.” Haya ni maneno ya Mungu.
Yesu anapiga hodi kwako - Wanawake wa Imani Kip. #3
Anakuita! Amekuja kukutafuta pale ulipo. Anabishahodi kwako. Si kwa jirani. Kwako. Anataka kuingia. Inaonekana kwamba haondoki mara akiona hakuna jibu. Ana haja kweli, na anaendelea kupiga hodi.
- Mpendwa msikiliaji – Umemsikia? Tega sikio sasa, umsikie leo.
Mwanamke Msamaria anawekwa huru na Yesu - Kip #4
Mwanamke tutakayemkuta leo alikuwa anatafuta upendo, uhuru na amani kama tulivyoongea kipindi kingine, sisi wote tunatafuta mambo haya juu ya mambo yote mengine. Lakini huyu mwanamke pale alipoangalia na kutafuta, hakuweza kuyapata. Labda pia wewe uko kwenye hali ya kutafuta sana upendo, uhuru na amani, lakini baado hujayapata vizuri. Labda unaangalia mahali ambapo haipo!