Yesu anapiga hodi kwako - Wanawake wa Imani Kip. #3
Anakuita! Amekuja kukutafuta pale ulipo. Anabishahodi kwako. Si kwa jirani. Kwako. Anataka kuingia. Inaonekana kwamba haondoki mara akiona hakuna jibu. Ana haja kweli, na anaendelea kupiga hodi.
- Mpendwa msikiliaji – Umemsikia? Tega sikio sasa, umsikie leo.
Mwanamke Msamaria anawekwa huru na Yesu - Kip #4
Mwanamke tutakayemkuta leo alikuwa anatafuta upendo, uhuru na amani kama tulivyoongea kipindi kingine, sisi wote tunatafuta mambo haya juu ya mambo yote mengine. Lakini huyu mwanamke pale alipoangalia na kutafuta, hakuweza kuyapata. Labda pia wewe uko kwenye hali ya kutafuta sana upendo, uhuru na amani, lakini baado hujayapata vizuri. Labda unaangalia mahali ambapo haipo!
Ushuhuda wa Dorena Jakobo 1/2 - Wanawake wa Imani kip. #5
Dorena Jakobo, "Mama Eliyah", alilelewa katika familia ya kipagani, lakini yeye na dada yake walivutwa na mambo ya kanisani. Na bila wazazi kujua, wakaenda kusali na baadaye wakabatizwa. Lakini hata kama aliokoka wakati wa utoto, Dorena alipokua, alikuja kuishi nyuma ya Neno la Mungu, na kukaa katika ndoa mbaya.
Ushuhuda wa Dorena Jakobo 2/2 - Wanawake wa Imani
Dorena Jakobo, "Mama Eliyah", ni mtoto mdogo katika familia yake na amekutana na vikwazo vingi maishani, hata hivyo, baba yake mzazi aliokoka kupitia yeye.
Sikiliza na utabarikiwa na ushuhuda wa Dorena Jakobo.