Maisha Mazuri kwa Watoto
Hutoa msaada thabiti kwa sisi sote tunaowalea watoto. Upendo pasipo mashartini mbinu ya msingi, lakini pia kukaa pamoja kunakojenga, nidhamuna mbinu nyinginezo zinafafanuliwa kwa makini. Kila atakaye kuwapa watoto wake maisha yaliyo na maendeleo yenye afya, yampasa akisome.
Msingi wa Imani
Ni hazina kubwa kwa wote wanaotaka kufahamu ukweli wa Imani ya Kikristo. Kimeandikwa na profesa wa theolojia mwenye fokasi ya Kiinjili na kwa lengo la kumwezesha msomaji kushuhudia, Namjua yeye nimwaminiye! Ni kitabu cha lazima kwa kila aliye na huduma ya kufundisha kanisani.
Roho Mtakatifu
Kuna maoni mengi kuhusu Roho Mtakatifu na kazi yake maishani mwetu. Kama ukitaka kujikita katika ukweli wa Biblia, kitabu hiki kitakusaidia.
Onjeni Bwana alivyo mwema
Kitabu hiki ni msaada wa kushiriki sakramenti ya Chakula cha Bwana kwa manufaa zaidi. Maelezo ya aina tatu: rahisi, ya kibiblia na ya kitheolojia.
Msingi wa imani
Ukitaka ‘mafuta’ ya mafundisho ya profesa kuhusu imani ya Kikristo, soma kitabu hiki! Cha lazima kwa wachungaji na walimu wa imani.