Michezo ya redio, podcast Anne Gihlemoen Michezo ya redio, podcast Anne Gihlemoen

15. Mkuu wa Amani 4

Yesu akazaliwa! Sikiliza kipindi hiki kujua zaidi kuhusu wageni waajabu waliowatembelea Yusufu na Mariamu baada ya Yesu kuzaliwa.

Urithi wa Adamu - Mkuu wa Amani 4
Hammerson Luhanga na Roger Gihlemoen

Wakati wachungaji wale wa makondeni wakianza safari kufuatia ujumbe wa Malaika. Yusufu alikuwa na wakati mgumu nje ya zizi la mifugo katika Bethlehemu, mara akae chini mara ainuke atembee aende huku na kule.... alihaha jasho jembamba likimtoka. Hatimaye akasikia sauti ya mtoto mchanga akilia sana. Yesu akazaliwa! Sikiliza kipindi hiki kujua zaidi kuhusu wageni waajabu waliowatembelea Yusufu na Mariamu baada ya Yesu kuzaliwa.

MkuuWaAmani_Radio_15.jpg
Read More
Michezo ya redio, podcast Anne Gihlemoen Michezo ya redio, podcast Anne Gihlemoen

14. Mkuu wa Amani 3

Yusufu na mkewe Mariamu walikuwa wanahangaika kutafuta mahali atakapozaliwa Mfalme mpya mwokozi wa ulimwengu ajaye kutimiza mpango wa Mungu.

Urithi wa Adamu - Mkuu wa Amani 3
Hammerson Luhanga/Roger Gihlemoen

Wakati msafara wa ngamia wa wachunguzi wanyota ukiifuata nyota, nyota inayowaongoza  toka uajemi na kusimama katika mji wa Bethlehemu mahali ambapo wanategemea watamuona mfalme mpya atakayekuwa mwokozi wa ulimwengu, Yusufu na mkewe Mariamu walikuwa wanahangaika kutafuta mahali atakapozaliwa Mfalme mpya mwokozi wa ulimwengu ajaye kutimiza mpango wa Mungu.Sikiliza kipndi hicho kujua nini itatokea.

MkuuWaAmani_Radio_14.jpg
Read More
Michezo ya redio, podcast Cathbert Msemo Michezo ya redio, podcast Cathbert Msemo

3. AGANO 1

Safari ya Abramu kwenda nchi aliyoahidiwa na Mungu. Sehemu ya kwanza

Urithi wa Adamu - Agano 1
Hammerson Luhanga na Roger Gihlemoen

Safari ya Abramu kwenda nchi aliyoahidiwa na Mungu ilikuwa ndefu yenye misukosuko na vikwazo vingi. Ilimchukuwa miaka kadhaa kufika nchi aliyoahidiwa na Mungu. Usiku mmoja Abramu alikuwa nje ya hema lake jangwani na kundi kubwa la watu aliofuatana nao kutoka vitani wakijenga hema kufanya makazi yao hapo. Abramu alitoka kwenye vita kuwakomboa ndugu zake. Alifanikiwa lakini alipata jeraha mguuni. Sikiliza kipindi hiki ujifunze mengi kuhusu Agano.

Agano_Radio_03.jpg
Read More