Soma habari mpya kutoka Soma Biblia

Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO LA 3/2022 linapatikana

Toleo hili la Riziki linaongozwa na mada isemayo “Tumeitwa kutenda mema”. Msingi wa mada hii unatokana na ukweli kwamba tunaishi katika nyakati ambazo ukatili na kutokuthaminiana kumekuwa kwa kiwango cha juu sana. Lakini pia majadiliano yanaenda zaidi, maana kutenda mema peke yake hakutoshi kama una tarajio la kuurithi uzima wa milele.

Bonyeza HAPA kusoma bure

Read More
Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO LA #2/2022

Katika toleo hili la Riziki tunajadili mada isemayo, Je, Mungu anaweza kumwacha mwanadamu? Msingi wa swali hili unatokana na hali ambazo tunakutana nazo kwenye maisha. Kuna wakati unapita mahali pagumu na kufikia hatua ya kufikiri kwamba Mungu amekuacha. Bila shaka, wakati wa shida na uhitaji mkuu ungetamani kuona mtu unayehusiana naye vyema akiwa karibu nawe kukutia moyo na kukusaidia. Vipi usipomwona, unajisikiaje?

Karibu kusoma zaidi Hapa bure

Read More
Magazeti, Twende Cathbert Msemo Magazeti, Twende Cathbert Msemo

Twende toleo #2/2022

Katika toleo hili tunajifunza juu ya 'Kukaza Mwendo'. Kupitia makala mbalimbali tutajifunza maana hasa ya kukaza mwendo kwenda Mbinguni, na zaidi tuta-elewa kuwa sisi ni washindi tunaoweza kuzishinda changamoto za dunia hii kwa sababu yupo mmoja ambaye anatuwezesha kushinda tukiwa naye.

Kuna kibonzo kitakachokufurahisha na kukufundisha kukaza mwendo bila kukata tamaa hadi kufikia ushindi. Usisahau dada Rehema! Ana michezo na ukijibu maswali vizuri unapata zawadi. Pia Kaka Kalamu anakukumbusha kumwandikia kama una swali, naye atakujibu. Karibu tusome!

Read More
Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO LA 04/2021

Katika toleo hili la Riziki tunajadili kuhusu nguvu ya msalaba. Ni mahali ambapo Yesu Kristo alitundikwa yapata miaka elfu mbili iliyopita, lakini tukio lile lilisababisha mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu. Ni tukio hili ambalo lilirudisha uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Yeye ambaye hapo kwanza alikuwa amegombana na Baba yake wa mbinguni, sasa amerudishiwa nafasi yake kama mtoto na mrithi pamoja na Kristo.

Read More
Watoto, Magazeti, Twende Cathbert Msemo Watoto, Magazeti, Twende Cathbert Msemo

TWENDE TOLEO LA #03/2021 'Linapatikana'

Katika toleo hili la Twende tutajifunza zaidi kuhusu agano letu na Mungu. Ndiyo, hata sisi tunaweza kufanya agano na Mungu. Ubatizo wa Kikristo ni agano la aina hii. Vilevile utasoma kuhusu watoto waliomwahidi Mungu jambo fulani. Kama una swali kuhusu agano, karibu kumwandikia Kaka Kalamu. Yuko tayari kujibu, mia kwa mia! Karibu kununua katika maduka ya Soma Biblia kwa Tsh. 500/= tu.

Read More
Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo

RIZIKI toleo la 02/2021 'Usitutie majaribuni, Utuokoe na yule mwovu' linapatikana

Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya nne, Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Mikononi mwa Mu-ngu majaribu yanaweza kuimarisha imani yetu na kutupa uzoefu kwamba Mungu ni mwaminifu na mwenye uwezo wa kutupitisha salama kiroho. Tunapopatwa na majaribu, kisha tukavuka salama, imani yetu huwa inaongezeka. Yesu anatuombea kila wakati; tulindwe na yule mwovu. Lengo la ombi hili ni kwamba, hata katikati ya majaribu, tulindwe dhidi ya hila za yule mwovu na tuvuke salama.

Ndani ya toleo hili utakutana na watu waliopita katika majaribu yaliyogusa kila eneo la maisha yao. Hata hivyo walisimama katika imani, na hatimaye walitoka wakiwa kama dhahabu safi ing’aayo. Siri yao ikoje? Soma makala za toleo hili, na ujifunze – kwa ajili ya maisha yako mwenyewe ili uweze kuwasaidia vema wanaojaribiwa!

Read More
RIZIKI, Magazeti Cathbert Msemo RIZIKI, Magazeti Cathbert Msemo

RIZIKI toleo la 01/2021 'Utusamehe makosa yetu' linapatikana

Ufafanuzi wa Sala ya Bwana unaendelea katika toleo hili la Riziki. Tumefikia sehemu ya tatu, Utusamehe makosa yetu, kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea. Msamaha ni jambo lenye nguvu sana. Tunapenda sana msamaha, lakini mara nyingi tunapotakiwa kukiri makosa yetu au kuwasamehe waliotukosea, tunaliona kuwa jambo gumu. Tunapenda kupokea msamaha lakini hatupendi kuutoa.

Read More
Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO #4/2020 'Utupe leo riziki yetu'

Toleo hili la RIZIKI ni muendelezo wa kuangalia Sala ya Bwana, sehemu ya pili isemayo “Utupe leo riziki yetu”. Sehemu hii inatufundisha kumwendea Mungu kwa moyo wa unyenyekevu na kumtegemea, tukimwomba atupe riziki yetu ya kila siku. Tunatiwa moyo tupeleke mahitaji yetu yafahamike kwa Mungu, tukiamini kuwa tutapewa. Kwa kuomba hivi tunakubali kwamba, kila tunachohitaji kwa ajili ya maisha yetu ya leo ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Read More
Twende, Watoto, Magazeti Cathbert Msemo Twende, Watoto, Magazeti Cathbert Msemo

Twende Toleo la #4, 2020 linapatikana

Karibu kununua TWENDE kwa Tsh. 500 tu katika maduka ya Soma Biblia. Toleo hili linafafanua juu ya Uhusiano wetu na Mungu. Kwa njia ya simulizi na hadithi nzuri utaweza kuelewa juu ya jambo hili. Utakutana pia na Dada Rehema na wenzake, na kuna michezo ya kuvutia. Usisahau kututumia majibu yako kama ilivyoelekezwa kwenye uk.5 na nyuma ya gazeti.

Read More
RIZIKI, Magazeti Cathbert Msemo RIZIKI, Magazeti Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO LA 3/2020 'SALA YA BWANA - Bwana, utufundishe kuomba'

Katika toleo hili la RIZIKI tunaanza na mfululizo wa makala kuhusu Sala Kuu au Sala ya Bwana. Sala hii inatufundisha kuwa sifa zote, heshima na utukufu ni kwa Mungu wetu peke yake. Kazi yetu katika maisha ya hapa duniani na hata kifoni ni kumletea Mungu utukufu kwa kila tufanyalo. Sala hii ambayo unaweza kuiomba chini ya dakika moja inatuonyesha ukuu, urefu, upana na kina cha upendo wa Mungu kwetu kupitia Yesu Kristo.

Read More
Magazeti, Twende Cathbert Msemo Magazeti, Twende Cathbert Msemo

Twende toleo la 2/2020 linapatikana

Ninakukaribisha usome makala zote na ujifunze mambo mazuri ya kujenga imani yako. Nikuambie! Mwaka huu Rehema atatoa zawadi kwa watoto watakaojibu vizuri maswali katika uk.5 na 6. Tazama katika ukurasa wa nyuma wa gazeti jinsi unavyoweza kutuma majibu yako. Majibu yako yakiwa sahihi, una kura moja. Tarehe 31/3, 30/6, 30/9 na 31/12 Rehema atatoa kura 15, yaani, kila mara kuna washindi 15 watakaozawadiwa.

Read More
Magazeti, Uinjilisti Cathbert Msemo Magazeti, Uinjilisti Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO LA 2, 2020 'Sifa za Kiongozi Bora'

Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna tunavyoweza kufikia maisha kwa kuandaa viongozi walio bora kuanzia katika umri wa ujana. Nia ni kuliamsha kanisa kama taasisi muhimu na ya kuaminika katika kuandaa viongozi wenye hofu ya Mungu, wenye maadili mema, wachapa kazi na walio tayari kuacha maslahi yao kwa ajili ya wengine.

Read More
Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO LA 1, 2020 'Ujenzi wa Familia Imara'

Katika toleo hili la RIZIKI tunaangalia mada isemayo, “Ujenzi wa familia imara”. Lengo ni kuibua na kujadili changamoto zilizopo kwenye taasisi hii muhimu ambayo mwanzilishi wake ni Mungu mwenyewe pale bustani ya Edeni. Ni wito wa kuliamsha kanisa na jamii yote, kuwa taasisi hii inapaswa kulindwa, kuimarishwa na kupiganiwa kwa nguvu zote.

Read More
Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo Magazeti, RIZIKI Cathbert Msemo

RIZIKI TOLEO 4/2019 linapatikana "JE! YESU AMEPOTEA NJIA?"

Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili kurudi kwa Yesu kama alivyoahidi. Lengo ni kusaidiana kama kanisa kupeana maarifa yenye uhakika juu ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Malengo ni wazi: Kwanza, tuwe na mafundisho sahihi kuhusu kurudi kwa Yesu. Pili, tuepukane na mafundisho ya uongo kuhusu jambo hili. Na tatu, tusije tukakata tamaa kuwa Kristo harudi, kisha tukalegea katika kuitenda kazi ya Mungu. 

Read More