Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
NDOA YENYE FURAHA
Usijinyime furaha ya kuwa na kitabu hiki kama msaidizi wako katika kazi uliyo nayo ya kufundisha mambo ya ndoa. Mwandishi mmoja wa Ndoa Yenye Furaha ni Askofu Blaston Gaville, KKKT Dayosisi ya Iringa, ambaye ana uzoefu mwingi wa kuwafundisha na kuwashauri wanandoa.
RIZIKI TOLEO 4/2019 linapatikana "JE! YESU AMEPOTEA NJIA?"
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili kurudi kwa Yesu kama alivyoahidi. Lengo ni kusaidiana kama kanisa kupeana maarifa yenye uhakika juu ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Malengo ni wazi: Kwanza, tuwe na mafundisho sahihi kuhusu kurudi kwa Yesu. Pili, tuepukane na mafundisho ya uongo kuhusu jambo hili. Na tatu, tusije tukakata tamaa kuwa Kristo harudi, kisha tukalegea katika kuitenda kazi ya Mungu.
TWENDE TOLEO LA 4/2019 Linapatikana
Mtoto mwenzangu, toleo hili lina habari njema kuhusu maisha yetu ya sasa na ya baadaye. Tutambue kwamba tukiwa ndani ya Yesu tutakuwa salama sasa na siku zijazo, na hata tukifa tutaenda kuishi na Yesu kwa furaha mbinguni.
Neno la leo
Neno la Leo ni kitabu cha kubeba popote. Mistari 4 ya Biblia inatoa mwanga kila siku.
Soma Biblia kila siku 2020
Soma Biblia kila siku 2020 ni Kalenda kamili na ufafanuzi kila siku kwa somo la Biblia
TWENDE toleo la 3, 2019 linapatikana
Habari hii njema tunafafanua zaidi katika toleo hili. Na wewe Kijana mpendwa, usisahau kuna makala nzuri kwa ajili yako pia. Inahusu miiba. Lakini Yesu yupo kukulinda isikuchome!
RIZIKI TOLEO LA 3, 2019 'TUNATAMBUAJE NAFASI YA WATOTO NA VIJANA NDANI YA KANISA?'
Je, wewe ni mtumishi wa Kanisa? Riziki toleo la Tatu mwaka 2019 linapatikana sasa.
Katika toleo hili la RIZIKI tunajadili namna ya kutambua nafasi ya watoto na vijana ndani ya kanisa. Nia ni kukumbushana kama kanisa umuhimu wa kuwatambua, ili tuwalee vizuri na kuwajali pamoja na vipaji walivyo navyo.
TWENDE TOLEO LA 2, 2019 Linapatikana
Umewahi kusikia mtu akisema, “Mimi ni mwanafunzi wa Yesu”? Au, “Mimi ni mtoto wa Yesu? Au, “Mimi ni mtumishi wa Yesu? Je, ana maana gani hasa? Soma makala za gazeti hili upate ufafanuzi mzuri kuhusu swali hili.
RIZIKI TOLEO LA 2, 2019 - 'UMISIONI WA NDANI'
Katika toleo hili la Riziki tunajadili kuhusu umisioni wa ndani. Lengo ni kukumbusha juu ya Utume mkuu wa Bwana Yesu wa kwenda kuhubiri habari njema ya toba na ondoleo la dhambi kwa wale ambao hawajafikiwa na injili.
Mpango wa kusoma Biblia kila siku kupitia Bible.com
Je, unajua kwamba mpango wetu wa kusoma Biblia kila siku inapatikana kupitia Bible App?
TWENDE TOLEO LA 1, 2019 Linapatikana
Karibu usome gazeti hili linalofafanua kuhusu safari yetu ya kwenda mbinguni. Linauzwa katika Maduka yote ya Soma Biblia na kwa dereva wetu wa mauzo anayezunguka na gari la kuuza vitabu na Biblia. Ni bei poa kabisa
RIZIKI TOLEO LA 1, 2019 - 'Ukristo ni utamaduni au imani?'
Katika toleo hili la RIZIKI tunachunguza kama Ukristo ni imani au utamaduni. Nia ni kukumbushana kuwa, mapokeo ya dini yanaweza kuwa mazoea au taratibu tupu zisizo na faida. Kama mwandishi mmoja alivyoandika, ndivyo taratibu zilivyo kama misingi yake haikujengwa katika Kristo. Lakini vilevile tamaduni na mapokeo zitafaa, tena zitakuwa na faida, kama zinatuelekeza kumwamini Yesu na kufanya mapenzi yake. Karibu usome toleo hili
Furahia mpango wa kusoma Biblia 'Soma Biblia Kila Siku 1'
Soma Biblia kila siku 1 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa kutoka Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
Twende toleo la 4, 2018 linapatikana
Gazeti hili maalum kwa watoto na vijana linazungumzia maana ya Amani kwa Wakristo. Amani ni usalama, raha moyoni na raha ya kutenda. Ni toleo la 4 kwa mwaka 2018 na lipo madukani Soma Biblia. Karibu umnunulie mtoto zawadi hii idumuyo na yenye kubeba mafundisho ya Neno la Mungu.
Riziki toleo la 4, 2018 - "Namwamini Roho Mtakatifu"
Katika toleo hili la RIZIKI tunaangalia sehemu ya tatu ya Imani ya Mitume inayoanza kwa kusema, Namwamini Roho Mtakatifu. Tunaamini yaliyomo katika toleo hili yataimarisha imani yako katika kumwamini Roho Mtakatifu.
Kitabu Kipya 'Ukalifa au Mauti' Kinapatikana
Ukalifa au Mauti ni kitabu kinachosimulia habari za kuteswa kwa Wakristo wa Nigeria. Ni toleo jipya kabisa la kiswahili. Karibu kupata nakala yako katika maduka ya soma biblia hapa Tanzania.
SIKU KUU YA MIKAELI NA WATOTO IMEKARIBIA
Ni furaha yetu kuona jinsi Kanisa linavyoweka siku kuu ya pekee kwa ajili ya watoto. Soma Biblia tunapenda kushiriki katika kazi ya kuwajenga watoto katika imani ya Kikristo kwa njia ya vitabu, Biblia na majarida kwa ajili ya watoto. Kwa hiyo tunatoa ofa maalum kwa sharika zote zinazopenda kuwapa watoto wao zawadi kwaajili ya siku kuu ya watoto.
Twende toleo no. 3, 2018 linapatikana sasa
Mpendwa msomaji wa Twende, uvumilivu ni tunda la Roho tunayepewa tunapomwamini Yesu. Biblia inatufundisha uvumilivu kupitia watu mbalimbali. Toleo hili limefafanua zaidi maana ya uvumilivu kwetu sisi Wakristo. Jipatie nakala yako kutoka Soma Biblia.
Namwamini Yesu Kristo - RIZIKI toleo la 3 2018
Toleo hili la RIZIKI tunaangalia sehemu ya pili ya Imani ya Mitume; Namwamini Yesu Kristo. Tunakumbushana kwa kutafakari maana ya maneno haya. Tunapokiri kwamba namwamini yesu, ina maana maisha yetu yamejengeka ndani ya msingi ambao ni Yesu Kristo.
TUMEJIFUNZA NA TUMEBURUDIKA - SEMINA YA WATUMISHI WA SOMA BIBLIA
Mwaka huu wafanyakazi wa Soma Biblia tulipata nafasi ya kukutana kwa pamoja katika kituo cha Mikutano cha Amabilis, mjini Morogoro kuanzia tarehe 23 hadi 27 Mei 2018. Wafanyakazi wa vituo vya Soma Biblia toka Arusha, Dar es salaam, Iringa, Mbeya na Mwanza walihudhuria semina hiyo. Pia tulikuwa na waendesha mada mbalimbali toka Chama cha Biblia Tanzania, na Mchg Oswald Ndelwa kutoka Iringa, ambaye aliendesha somo la Biblia kwa siku mbili.