Soma habari mpya kutoka Soma Biblia
"Tumwabudu Mungu Wetu" inapatikana sasa
Toleo jipya la Tumwabudu Mungu Wetu linapatikana sasa.
"...mwishindanie imani"
Je, nini itatokea kwa imani yetu, ikiwa kila kizazi huibadilisha tu kulingarna na mawazo, mahitaji na mipango yake? Katika RIZIKI toleo la kwanza 2018, tutaangelia zaidi maneno muhimu kuhusu Imani yetu ya Kikristo.
Mwongozo wa kusoma Biblia kwa kudownload
Msaada wa kugundua hazina katika Neno la Mungu. Karibu kuidownload hapa.
Shindano la uandishi wa kitabu kwa vijana
Soma Biblia hushiriki katika wito wa kuwaletea vijana habari njema ya Biblia kuhusu Yesu Kristo ili wamwamini na kumfuata. Kwa hiyo tunawakaribisha wote wenye vipawa vya uandishi waandike kitabu kwa vijana wenye umri wa miaka 13-19.
"Imani ijaribiwapo" - RIZIKI toleo #3, 2017
Mimi na wewe tunaweza kuwa na maswali mengi yanayosumbua imani yetu kututilia wasiwasi mwingi wa kiroho.
Siku kuu ya watoto
SIKU YA MIKAELI NA WATOTO INAKARIBIA. Soma Biblia inapenda kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa watoto bega kwa bega na Kanisa. Kwa hiyo tunatoa ofa maalum kwa sharika zote zinazopenda kuwapa watoto wao zawadi kwa ajili ya siku kuu ya watoto.
Taarifa mpya kutoka kwa Soma Biblia
Miezi iliyopita tumekuwa busy sana hapa Soma Biblia. Tumechapa matoleo jipya ya Twende na RIZIKI, tumefanya semina ya wafanyakazi wote, na kitabu kipya kimetolewa. Karibu kusoma zaidi!
YESU NI FIDIA - RIZIKI Toleo jipya
Yesu ni Fidia - kwa tafsiri rahisi neno fidia lina maana ya gharama ambayo inatolewa kwa ajili ya kufanya ukombozi. Yesu amelipa gharama yote kwa ajili yetu wanadamu. Hii ina maana gani hasa kwetu?
Kumbukumbu ya ”Mzee JJ”, Jon Jøssang 30.10.1926-30.12.2016
Kwa majonzi makubwa tunasikitika kutangaza kifo cha mwanzilishi wa Scripture Mission, Mzee Jon Jøssang. Mzee Jøssang amefariki tarehe 30 desemba, 2016 huko Norway alipokuwa akiishi na familia yake. Jøssang amefariki akiwa mzee wa umri wa miaka 90.
"Miujiza katika mpango wa Mungu"
RIZIKI toleo la 4 linapatikana sasa. Karibu kusoma kuhusu Miujiza katika mpango wa Mungu.
Duka la Soma Biblia Arusha – eneo jipya
Tarehe 14/11 Duka la Soma Biblia Arusha lilihamia eneo jipya.
"Majina ya Mungu", RIZIKI toleo la tatu
Majina ya Mungu yametumika ndani ya Biblia kama mwongozo wa kujifunza tabia ya Mungu. Toleo hili la RIZIKI linaeleza zaidi.
TWENDE Toleo la Tatu
Mwokozi wa ulimwengu:
Ni mmoja anayeokoa watu kutoka kifo na magonjwa. Ni mmoja anayeweza kufanya amani. Ni mmoja mkubwa na hodari, na mwenye nguvu zaidi ya shujaa!
Katika yeye tuna Ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi
Ukombozi, maana yake ni kwamba wewe umefunguliwa kwa sababu gharama ya uhuru wako imelipwa.